Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 11:17

Wataalamu washauri njia ya kukabiliana na upungufu wa fedha za kigeni


Rais Tanzania Samia Suluhu akiwa Dodoma tarehe 22 Aprili , 2021. Picha na AFP.
Rais Tanzania Samia Suluhu akiwa Dodoma tarehe 22 Aprili , 2021. Picha na AFP.

Wataalamu wa uchumi nchini Tanzania wameitahadharisha serikali yao kuwa na utaratibu wa kuzalisha bidhaa bora ambazo zitaweza kuuzika nje ya nchi kwa wingi ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa fedha za kigeni, hasa dola.

Wataalam wanaeleza kuwa fedha hizo zinahitajika kwa ajili ya manunuzi na mauzo ya bidhaa kutoka nje.

Fedha za kigeni nchini Tanzania zimeadimika hali iliyopelekea thamani ya dola kupanda na kuuzwa kwa gharama ya juu ya shilingi 2,499 hadi shilingi 2,535 kutoka shilingi 2,410 hadi shlingi 2,015 mwezi uliopita.

Mshauri wa uchumi

Mshauri wa uchumi, fedha na kodi kutoka Dar es Salaam Ahobokile Mwaitenda amesema hali hiyo inasababishwa na Taifa kununua bidhaa zaidi kutoka nje pamoja na kuchukua mikopo bila ya kuwa na mikakati ya kiuchumi itakayozalisha bidhaa nyingi kuuzwa nje.

Mwaitenda anaeleza: "Sisi tunanunua zaidi nje tunakopa zaidi kuliko jinsi ambavyo tunaweza kuuza zaidi nje na jinsi ambavyo tunaweza kupata mitaji ya kutoka nje kuja kwenye uchumi wetu."

Aidha kuongeza uzalishaji na kuuza bidhaa nje ya nchi kwa kiasi kikubwa ni moja ya njia nzuri ya kudhibiti hali ya uchumi na kuingiza fedha za kigeni kwa Taifa. Hii inajulikana kama sera ya kukuza biashara ya nje au sera ya biashara ya kimataifa.

Mtafiti wa uchumi

Kwa upande wake Azizi Rashidi ambaye ni mtafiti wa masuala ya uchumi wa fedha na benki kutoka Dar es Salaam amesema kuwa njia bora ya serikali kudhibiti hali hiyo ni kuwa na uchumi unaozalisha bidhaa za kupeleka nje ya nchi kwa kiasi kikubwaa ambazo zitapelekea kuingiza fedha nyingi za kigeni kwa Taifa.

Rashidi anaeleza: "Kwahiyo njia kubwa na nzuri kabisa naweza kusema inaweza kutupunguzia tatizo ni kuwa na uchumi unaozalisha na kupeleka nje ya nchi kwa kiasi kikubwa kukuza sekta za uuzaji nje ya nchi ambazo ndio zitatuletea hela nyingi za kigeni kama ni kilimo tunauza bidhaa ghafi za kilimo tuzichakate hapa ndani gunia moja ukiuza laki moja ukiuza korosha ambayo imeshatengenezwa utaiuza gunia moja pengine hata laki tatu kwahiyo ile hela ya fedha ya kigeni unayopata itaongezeka zaidi.

Mtaalam wa Uchumi

Hata hivyo mtaalamu wa uchumi kutoka Dar es Salaam Joshua Lukonge amesema ili kupambana na hali hii taifa linatakiwa kuepuka kutumia dola ambayo ni adimu na kuacha kununua bidhaa za nje ambazo zingeweza kuzalishwa ndani.

Naye Lukonge anafafanua: "Hakuna ulazima wakutumia dola ambayo ni hadimu sana kununua bidhaa ambazo tungeweza kuzizalisha ndani kwahiyo maana yake kama kuna bidhaa ambazo kama zinaweza kununuliwa hapa ndani ya nchi hakuna ulazima wakuzinunua nje basi utaratibu ufanyike kama ni utaratibu wa kisheria ama wakisera wakuhakikisha hatununuwi bidhaa ambazo tunaweza kuzalisha ndani."

Ikumbukwe huko nyuma Benki Kuu ya Tanzania BOT kupitia Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tafiti za Uchumi na Sera BoT Dkt. Suleiman Misango imewahi kueleza kuwa mwenendo wa uchumi wa dunia umeathiri uchumi wao na hasa upatikanaji wa fedha za kigeni hapa nchini.

Amri Ramadhani Sauti ya Amerika Dar es Salaam

Forum

XS
SM
MD
LG