Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 07:57

Wataalam: Uhalifu wa mitandao wakua kwa kasi Afrika


Mfanyakazi akiwa kwenye maabara ya kutengeneza virusi katika makao makuu ya usalama wa mitandao wa kampuni ya Kaspersky, Moscow, Julai 29, 2013.
Mfanyakazi akiwa kwenye maabara ya kutengeneza virusi katika makao makuu ya usalama wa mitandao wa kampuni ya Kaspersky, Moscow, Julai 29, 2013.

Duniani kote, hatari inayotokana na uhalifu wa mitandao unaongezeka kukiwa na matukio yaliyo maarufu kama lile lililotokea hivi karibuni la shambulizi la kirusi kinacho julikana kama "Wannacry ransomware" ambao ni kielelezo cha kuongezeka kwa hatari hii.

"Ransomware" - kilikuwa ni kirusi kinachoambukiza kompyuta na kusababisha faili zisiweze kufunguka mpaka pale mmiliki wa faili hizo atakapolipa kikombozi.

Wataalamu wa mitandao wanasema kuwa Afrika ndio hasa iko katika hatari kwani matumizi ya intaneti na teknolojia ya simu zinaongezeka kwa kasi, wakati usalama wa mitandao katika bara hilo haulingani na kasi hiyo ya uhalifu.

Matumizi ya teknolojia katika bara la Afrika yanaongezeka kwa kasi kubwa. Biashara ya kwenye mitandao inatarajiwa kufikia thamani ya dola bilioni 75 ifikapo mwaka 2025. Lakini fursa kama hii inakuja na hatari zake, anasema mshauri wa usalama wa mitandao wa Uingereza William Kapuku-Bwabwa.

“Miundombinu ya usalama wa mitandao, bado nchi nyingi za Afrika hazijaweza kuwa nayo, na zile ambazo wameweza kuwa na miundombinu hiyo bado iko katika hatua ya mwanzoni kabisa," ameeleza Bwabwa.

Ripoti ya kampuni inayoshughulikia usalama wa mitandao (NORTON) inasema takriban watu wa Afrika Kusini milioni 9 wameeleza waliathiriwa na uhalifu wa mitandao mwaka 2016. Barani Afrika hii ni gharama kubwa, anasema Stephanie Itimi, mshauri wa biashara za mitandao Afrika.

“Bara la Afrika linapoteza zaidi ya dola za Kimarekani bilioni 2.5 kila mwaka kutokana na uhalifu wa mitandao. Na zaidi ya Dola za Marekani milioni 500 zinapotea huko Nigeria," ameeleza Itimi.

XS
SM
MD
LG