Ushindi huo unahitajika ili kuweza kutekeleza ahadi zao za mageuzi mkubwa waliotoa na kuweza kuingia madarakani miezi minane iliyopita.
Miongoni mwa ahadi hizo ni mageuzi ya kiuchumi, usawa wa kijamii na kupambana na rushwa.
Rais Bassirou Faye, alipata asili miami 54 za kura mwezi march na hivyo kuongeza matumaini ya idadi kubwa ya vijana wa taifa hilo la afrika Magharibi.
Faye na waziri mkuu wake Ousmane Sonko wanalazimika kukabiliana na ukuaji mdogo wa uchumi, ughali wa maisha, kupambana na ukosefu wa ajira miongoni hasa mwa vijana na kukabiliana na tatizo la idadi kubwa ya vijana wanaohatarisha maisha yao kuelekea Ulaya ili kutafuta maisha bora kila mwaka.
Vituo vya kupiga kura vinatarajiwa kufunguliwa saa mbili asubuhi ili kuwaruhusu wapiga kura milioni 7 walojiandikisha kupiga kura zao hadi saa mbili usiku.
Uchaguzi huo ni kugombania viti 165 vya bunge ambapo sehemu kubwa ya viti hivyo vilikua vinashikiliwa na wafuasi wa rais wa zamani Macky Sall tangu mwaka 2022.
Sall, akiwa uhamishoni na hasimu wa kisiasa wa Sonko kwa muda mrefu watapambana wakati wa uchaguzi huo watakapo ongoza orodha ya wagombea wa vyama vyao.
Muungano wa upinzani unaongozwa na Meya wa Dakar, Barthelemy Dias na Waziri mkuu wa zamani Amadou Ba, umekua na sauti kubwa wakati wa kampeni za uchaguzi huo wa Jumapili.
Kampeni hiyo imegubikwa na ghasia kati ya wafuasi wa chama tawala cha Pastef na upinzani huku Sonko akitoa wito kwa wafuasi wake walipize kisasi baada ya kile alichokieleza ni uvamizi wa wafuasi wake ulofanywa na wafuasi wa upinzani,
Forum