Nchi za Sahel za Mali, Burkina Faso na Niger zinakumbwa na uasi mbaya wa wanajihadi na zinaongozwa na wanajeshi waliochukuwa madaraka katika msururu wa mapinduzi tangu mwaka 2020.
Viongozi wa kijeshi katika nchi hizo tatu walivunja uhusiano na mataifa ya Magharibi na kujitenga na Jumuia ya uchumi ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) na kuunda shirikisho lao.
“Hali katika Sahel kwa kukabiliana na ugaidi inahitaji uhamasishaji wa kimataifa wa jumuia ya kimataifa,” alisema Faye, ambaye ni mpatanishi aliyeteuliwa na ECOWAS katika mazungumzo na mataifa hayo matatu.
Ameomba uungwaji mkono zaidi wa Umoja wa Ulaya, akisema “ inafahamika kwamba mabara ya Afrika na Ulaya yana mustakabali wa pamoja wa usalama”, wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
Sanchez alipongeza juhudi za upatanishi za Senegal katika kanda ya Sahel, akiongeza kuwa “ Kanda hii ni eneo muhimu la kimkakati kwa nchi yangu, na kwa hiyo tunataka kuchangia kwa utulivu na ustawi wake.”
Forum