Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 17:01

Wasanii wa Kiafrika washiriki Tamasha la Amani DRC


Waumini wa Kanisa Katholiki mjini Kindu, DRC
Waumini wa Kanisa Katholiki mjini Kindu, DRC

Wasanii kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika walitumbuiza kwenye tamasha la “Amani” lililofanyika mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kuwafariji waathirika wa mzozo licha ya ongezeko la ukosefu wa usalama katika eneo hilo.

Mashabiki walipiga makofi, walishangilia na kuimba pamoja na wanamuziki zaidi ya 20 akiwemo muimbaji nyota wa Senegal Didier Awadi ambaye aliuambia umati wa watu waliojaa furaha uliohudhuria hafla hiyo katika jiji la Bukavu kuwa "Dhamira yetu ni kuwa pamoja nanyi.”

“Tuna jukumu la kuonyesha mshikamano, kuwa upande wa watu wanaoshambuliwa” Awadi aliliambia shirika la habari la Reuters baada ya onyesho.

Tamasha la Amani, kwa kawaida hufanyika Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini. Lakini tamasha hilo lilihamishiwa sehemu nyingine kwa mara ya kwanza tangu lizinduliwe mwaka 2014, kutokana na mashambulizi ya kundi la waasi wa M23, ambao wamelikaribia jiji hilo mwishoni mwa wiki iliyopita.

Bukavu ni mji mkuu wa jimbo la Kivu Kusini, unaoonekana kuwa salama zaidi, licha ya kuwepo kwa makundi kadhaa yenye silaha. Zaidi ya watu 30,000 walihudhuria tamasha hilo, ambalo lilifanyika kuanzia Ijumaa hadi Jumapili.

-Chanzo cha habari hii inatoka shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG