Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 11:39

Tshisekedi alaani 'vita vya kikatili' nchini DRC katika mkutano wake na rais wa Comoros


Rais wa DRC Felix Tshisekedi
Rais wa DRC Felix Tshisekedi

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Alhamisi amelaani kile alichokiita “vita vya kikatili” vinavyoendelea mashariki mwa nchi yake, wakati wa ziara katika kisiwa kidogo cha Comoros.

Rais Felix Tshisekedi alifanya mazungumzo na mwenzake wa Comoros Azali Assoumani, ambaye anapigiwa upatu kuchukua urais wa zamu wa Umoja wa Afrika kutoka kwa rais wa Senegal wiki ijayo.

Tshisekedi alikuwa pia Angola mapema wiki hii kwa mazungumzo na Rais Joao Lourenco, ambaye ni mpatanishi wa Umoja wa Afrika kati ya DRC na Rwanda katika mzozo unaopamba moto mashariki mwa Congo.

“Kila mahali nilipokwenda nilizungumza kuhusu nchi yangu na vita hivi vya kikatili vilivyoshinikizwa kwetu na Rwanda,” Thisekedi amesema, akielezea matumaini yake kwamba Assoumani ataupa kipaumbele mzozo huo na kuweza kuleta amani huko.

DRC inaishtumu jirani yake Rwanda kuliunga mkono kundi la waasi la M23 katika mzozo huo.

Rwanda inakanusha madai hayo na inaishtumu DRC kushirikiana na kundi la zamani la waasi wa Kihutu wa Rwanda, FDLR, lililoanzishwa nchini DRC baada ya mauaji ya kimbari ya Watutsi wengi nchini Rwanda mwaka wa 1994.

XS
SM
MD
LG