Upigaji kura ulifanyika Alhamisi wakati huduma za simu za mkononi na mtandao zikisitishwa nchi nzima na kuwepo ghasia hapa na pale, ikichochea mashaka kuhusu matokeo ya uchaguzi na wasiwasi wa kuwa uchaguzi wa haki kutokana na utata uliokuwepo.
Tume ya Uchaguzi ya Pakistan ilitangaza matokeo machache ya kwanza mapema Ijumaa, saa 12 baada ya kumalizika upigaji kura nchi nzima ambapo watu takriban milioni 241 walishiriki.
Tume hiyo ilitangaza matokeo asilimia 24 tu hadi kufikia wakati wa mchana.
Matokeo haya yanaonyesha kuwa kikundi cha wagombea wakujitegemea, ambao wanaungwa mkono na Pakistan Tehreek-e-Insaf, au PTI, chama cha Waziri Mkuu wa zamani Imran Khan aliyefungwa, kilifanya vizuri kuliko kilivyotarajiwa licha ya kulengwa na kamatakamata iliyofanywa na serikali kabla ya uchaguzi.
Uchaguzi huo ulikuwa kwa ajili ya kugombea viti 266 Bunge la Taifa, katika baraza la Wawakilishi.
Wagombea wanaofungamana na PTI walikuwa katika ushindani mkali na wale wa chama cha Pakistan Muslim League – Nawaz, au PML-N, kinacho ongozwa na waziri mkuu wa zamani Nawaz Sharif, inaonekana kuwa jeshi lenye nguvu ndiyo linapendelea awe madarakani.
Chama cha Pakistan Peoples Party, kinachoongozwa na Bilawal Bhutto Zardari, kilikuwa kiko nyuma nafasi ya tatu.
Katika posti iliyochapishwa katika mtandao wa X, ambao ulikuwa zamani maarufu Twitter, Gohar Khan, anayekaimu uwenyekiti katika PTI, alidai chama chake kilikuwa kinaongoza kwa zaidi ya viti 150 lakini “kuna jaribio la kubadilisha matokeo.”
Msemaji wa PML-N Marriyum Aurangzeb alidai chama chake kilikuwa katika nafasi “yenye nguvu” na mwanamke huyo ataweza kuunda serikali huko Islamabad.
Kulingana na hisabu za wilaya ya upigaji kura, jumuisho la kura lisilokuwa rasmi kutoka vyombo vya habari vya Pakistani lilionyesha wagombea wanaoungwa mkono na PTI wakiongoza katika uchaguzi nchi nzima.
Katika baadhi ya maeneo, walikuwa wanaongoza kwa kura 30,000 hadi 50,000.
Hata hivyo, kulingana na matokeo rasmi ya awali yaliyotolewa Ijumaa, walikuwa wanashika mkia au kupoteza ushindi kwa kura chache.
Mabadiliko ya matokeo yanalaumiwa kutokana na kucheleweshwa kutangazwa kwake kile PTI kinadai ilikuwa kuhujumu matokeo.
“Matokeo yameshapangwa. Iwapo matokeo ya mwisho yataonyesha kitu chochote kuliko ushindi wa PTI, PTI itakataa matokeo na itakuwa ni wizi wa kura, na inaeleweka hivyo: Mafanikio yake ya awali yalipelekea ucheleweshaji wa saa kadhaa kutangazwa matokeo ya mwisho. Jeshi hili, linakusudia kuwanyima madaraka PTI, limeingilia kati mchakato huo,” alisema Michael Kugelman, mkurugenzi wa Taasisi ya South Asia katika Kituo cha Wilson, mjini Washington.
Tume ya uchaguzi ilitupa lawama katika kuandaliwa matokeo kuwa ni “tatizo la mtandao,” wakati Waziri wa Mambo ya Ndani alitetea umuhimu wa kusitishwa kwa huduma za simu za mkononi na intaneti siku ya uchaguzi, kuwa “ ni matokeo ya hatua za kuihami nchi zilizochukuliwa kuhakikisha usalama kamili” wa upigaji kura.
Huduma za simu na mitandao zilirejeshwa siku ya Ijumaa asubuhi.
Forum