Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 09:24

Pakistan: Vituo na wafanyakazi wa uchaguzi katika maandalizi ya mwisho


Kituo kimojawapo cha uchaguzi kikiwa katika maandalizi ya siku ya mwisho kabla ya uchaguzi kufanyika Alhamisi.
Kituo kimojawapo cha uchaguzi kikiwa katika maandalizi ya siku ya mwisho kabla ya uchaguzi kufanyika Alhamisi.

Vituo vya kupigia kura na wafanyakazi wa uchaguzi wanajitayarisha mjini Islamabad kabla ya uchaguzi wa bunge utakaofanyika hapo kesho Alhamisi.

Nchi inachagua bunge jipya wakati mashambulizi ya wanamgambo yameongezeka na kuweka giza nene katika upigaji kura na migawanyiko mikubwa ya kisiasa na kuonekana huenda kukawa na serikali ya mseto.

Uchaguzi umekuja wakati muhimu katika taifa hilo lenye nguvu za nyuklia, ambayo ni mshirika wa Magharibi anayepakana na Afghanistan, China, India na Iran eneo lenye mipaka yenye mizozo na mivutano ya uhusiano.

Serikali ijayo ya Pakistan, itakabiliwa na changamoto kubwa, kutokana na hali ya ghasia, ili kukabiliana na mzozo mkubwa wa kiuchumi ambao unatokana na uhamiaji haramu.

Maelfu ya polisi na vikosi vya jeshi wamepelekwa kwenye vituo vya kupiga kura kote nchini Pakistan kuimarisha ulinzi mkali.

Bado, katika siku ya mkesha wa uchaguzi, kulikuwa na mashambulizi mawili ya mabomu kwenye ofisi za uchaguzi katika jimbo la kusini maghairbi la Baluchistan ambapo watu 26 waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Vyama vya siasa karibu 44 vinawania kupata viti katika bunge lenye viti 266 ambavyo vinagombaniwa katika bunge la taifa.

Forum

XS
SM
MD
LG