Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 14:49

Wakulima wadogo wakabiliwa na changamoto za uzalishaji na usafirishaji miwa


Mfanyakazi akimwagilia shamba la miwa huko katika kampuni ya kuzalisha sukari ya Kenana (KSC) A worker irrigates a sugarcane plantation at Kenana kilomita 270 ( maili 170) kusini mwa Khartoum, Sudan, Mei 14, 2013
Mfanyakazi akimwagilia shamba la miwa huko katika kampuni ya kuzalisha sukari ya Kenana (KSC) A worker irrigates a sugarcane plantation at Kenana kilomita 270 ( maili 170) kusini mwa Khartoum, Sudan, Mei 14, 2013

Wakulima wadogo wa miwa huko Turiani, Morogoro, kusini magharibi mwa Tanzania, wanakabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi kutokana na changamoto katika uzalishaji na usafirishaji wa miwa kuelekea viwandani.

Pia hali hiyo ni pamoja na ucheleweshwaji wa pembejeo za kilimo na kusababisha athari kwa maisha yao na uzalishaji wa zao hilo muhimu. Amri Ramadhani anaripoti kutoka Turiani Morogoro.

Abisai William amekuwa akijishughulisha na kilimo cha miwa hapa Turiani, Morogoro kwa miaka mingi. William huuza miwa katika kiwanda cha Mtibwa ambacho huchakata miwa kwa kuzalisha sukari.

Hata hivyo kwa wakulima kama yeye changamoto ni nyingi. Anasema upatikanaji wa mbolea kwa kuchelewa ni miongoni mwa vitu ambavyo vinafanya uzalishaji wa miwa kuwa hafifu na usio na tija kwa wakulima wadogo.

William anaeleza kuwa: Mbolea kutokupatikana kwa wakati na pia tuseme sijui ni masuala ya viwanda au nini kwasababu wakulima wanakuwa na uhitaji wa mbolea lakini unakuta kipindi kile ambacho kuna uhitaji wa mbolea, mbolea haipatikaniki ikija kupatikanika mbolea miwa tayari imeshapitwa na wakati.

Maslahi madogo ni jambo lingine linalowakatisha tamaa. Wakulima hawa hufanya kazi kubwa kwa mshahara mdogo kama anavyosema Zozo Makengwa mfanyakazi anayshughulika na usafirishaji katika shamba la miwa.

Makengwa anasema kwamba: "Kwa serikali yetu hii kama kuna uwezekano wa kuweza kutuboreshea kwanza juu ya mazingira ya kipato kwasababu kipato kipo chini sana maisha sasahivi yapo juu sasa leo hii unalipwa tani shillingi mia sita halafu na tani boi unamlipa wewe mwenyewe hapo hapo unafikili umebeba trip moja toka asubuhi unapakia tani kumi na tano shingapi ukitoa ya tani boy unabaki na shingapi."

Kenneth Bengesi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania amesema ili kusaidia wakulima kuongeza uzalishaji wa miwa serikali imepitisha bajeti kupitia bodi ya sukari kwa ajili ya utengenezaji wa vitalu vya kuoteshea mbegu na wanaendelea kutafuta fedha ili kutengeneza miundombinu ya umwagiliaji katika mashamba ya wakulima wadogo wadogo.

Bengesi anafafanua: "Serikali kupitia bodi ya sukari mwaka huu imepitisha bajeti ya kuweza kusaidia wakulima kuwatengenezea vitalu vya mbegu na hii tutaanza na kilombero ambapo kwa msimu huu tutakuwa na kitalu cha mbegu cha hekta 400 ambapo tutaweza kuzalisha mbegu ambazo zitaweza kusambazwa kwa wakulima. Mbegu hizo zitakuwa ni safi na salama ambazo zitakuwa hazina magonjwa kuhakikisha kwamba wakulima wanaongeza tija.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa bodi ya sukari, kwa kipindi cha miaka mitano Tanzania imeongeza uzalishaji kutoka tani laki tatu na tano mpaka tani laki nne na sitini huku mahitaji ya nchi yakiwa ni tani laki nne na tisini kwa sukari ya matumizi ya kawaida na pakiwa na upungufu wa tani elfu thelathini kwa matumizi ya kawaida na tani laki mbili na arobaini kwa matumizi ya viwandani ambazo ndizo zinaagizwa kutoka nje ya nchi na hivyo kuigharimu nchi dola za marekani million 350.

Imetayarishwa na mwandishi wetu Amri Ramadhani, Morogoro, Tanzania.

Forum

XS
SM
MD
LG