Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 11:51

Wakulima Kenya wadai Mbolea za Kemikali zadhoofisha ardhi


Uwekaji wa mbolea katika shamba la chai huko Kenya
Uwekaji wa mbolea katika shamba la chai huko Kenya

Wakulima barani Afrika wanasema ardhi yao inadhoofika kutokana na mbolea yenye kemikali. Huku uzalishaji ukishuka kutokana na ardhi hiyo duni, watalaamu wanashauri kurejea katika mbinu za kiasili za kilimo ili kurejesha ubora wa ardhi na uzalishaji.

Makulima wa mboga, Benson Wanjala na mke wake wanafanyakazi ya kupalilia heka mbili za shamba lao nje ya viunga vya Nairobi.

Haya ni mabadiliko makubwa katika harakati za kilimo za miongo mwili na nusu iliyopita, wakati alipokuwa akilima shamba lake la heka kumi lililoko kwenye kijiji kimoja nchini Kenya.

Ardhi ya Wanjala ilikuwa ikimpatia kiwango kikubwa cha mavuno ya takriban magunia 200 ya mahindi kila msimu. Lakini idadi hiyo imekuwa ikishuka kadri miaka ilivyokwenda na kufikia magunia 30 tu.

Wanjala anailezea hali hii kuwa inatokana na mbolea yenye acidi ambayo waliwahi kuitumia, anaamini ardhi hiyo iliyowahi kuwa na rutuba sasa haina na hivyo anashindwa kuikimu familia yake.

Mjini Nairobi, shamba la mboga mboga la Wanjala awali lilionyesha hali nzuri. Lakini haraka aligundua kupungua kwa mavuno. Anadhani kwamba kuongezeka kwa matumizi ya mbolea ambayo si organiki kunachangia kushuka kwa ubora wa ardhi na uzalishaji.

Mfanyakazi akiwa amebeba mbolea ya asili katika kiwanda cha kutengeneza mbolea ya aina hiyo
Mfanyakazi akiwa amebeba mbolea ya asili katika kiwanda cha kutengeneza mbolea ya aina hiyo

Licha ya changamoto hizo, Wanjala anasema bado ana nia ya dhati ya kutengeneza maisha kupitia kilimo. Hadithi yake inaashiria mapambano makubwa ambayo wakulima wengi wanapitia katika kuboresha ubora wa aridhi ulioshuka.

Mtalaamu wa udongo na mtendaji mkuu wa Thea, kampuni inayojishughulisha na ubora wa udongo Priscilla Wakarera amesema

“Tuna kiwango kikubwa cha uharibifu wa udongo ikiwa ni matokeo ya mkusanyiko wa mbolea yenye madini ya chuma kwenye udongo kutokana matumizi makubwa ya aina za mbolea. Hii inafanya nini, ni kwamba inabadili pH ya udongo kuwa acidi, na pale udongo unapokuwa pH yenye acidi, mimea haiwezi kupata lishe nzuri iliyo kwenye udongo.”

Nchini Kenya, wakulima wengi wanapendelea mbolea aina ya DAP kwa ajili ya mahindi, lakini kuendelea kuitumia mara kwa mara kunapelekea acidi ya viwango vya juu katika udongo. Wakarera anasema upimaji udongo ni muhimu kuangalia viwango vya acidi kabla ya kuamua aina gani ya mbolea kuitumia.

Anasema matumizi yasiyo sahihi ya mbolea zenye kemikali, pamoja na mbinu duni za kilimo kama kilimo cha mazao ya aina moja na uwezekano mkubwa wa mbolea ambazo ni fake, zinachangia uharibifu wa udongo katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Waki Munyal akipeta mahindi baada ya mavuno
Waki Munyal akipeta mahindi baada ya mavuno

Wakulima wanasema fursa kwa upimaji udongo si wa kiwangokikubwa na unachukua muda mrefu, mpaka mwezi mmoja, ndiyo unaweza kupata majibu.

Kwa wakulima kama John Mburu Gitu, kupata msaada wa mtaalamu wa udongo kumemletea matokeo yenye tija. Gitu alishuhudia mavuno yakiongezeka katika shamba lake la avocado baada ya udongo kupimwa.

Greepeace Africa inashirikiana na wakulima wadogo wadogo ili kuongeza ufahamu kuhusu kipindi cha mpito kutoka kiviwanda mpaka mbinu kilimo endelevu.

Wanazisihi serikali kupitisha sheria ambazo zitasaidia mbinu za kilimo endelevu na kuwapatia maafisa fursa ya kusaidia katika kipindi cha mpito.

Idara ya Chakula na Kilimo inaripoti kuwa uzalishaji mahindi Kenya umeshuka kwa asilimia 4 na kufikia tani milioni 44 mwaka 2022, ikimaanisha kuwa uagizaji kutoka nje uliongezeka ili kukabiliana na upungufu.

Suala la kushuka kwa uzalishaji kilimo si Kenya Kenya peke yake, maeneo mbalimbali ya Afrika, bara lenye asilimia 65 ya aridhi duniani yenye rutuba na haijalimwa. Lakini inatumia takriban dola bilin\oni 60 kwa mwaka kuagiza chakula kutoka nje ili kukidhi mahitaji, kwa mujibu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika.

Forum

XS
SM
MD
LG