Kati ya wakimbizi hao (watoto), 570 walitenganishwa na wazazi wao kutokana na kuanza kwa vita na kukimbilia maeneo tofauti na wengine 159 wamepoteza mawasiliano na ndugu zao ambao walikuwa wakikaa nao kabla ya vita kuanza.
Watoto ambao wako kwenye upweke ni wenye umri kati ya miaka minne na kumi na saba.
Kwa mujibu wa kamanda wa makazi ya wakimbizi ya Palabek David Wangwe, watoto hao wamekabidhiwa kwa wazazi wa kufikia ambao wanawangalia kwa hivi sasa.
“Resheni za chakula na mahitaji mengine yaliyokusudiwa kwa watoto hao yanatolewa kwa wale walipewa jukumu la kuwatunza watoto hao.
Vyanzo vya habari nchini Uganda vimesema kuwa mipango iko njiani amesema Wangwe kutoa vifaa vya kujifunzia kwa watoto hao ili shule zitakapo funguliwa waweze kuanza masomo.
Repoti ya Umoja wa Mataifa
Wakati huo huo Repoti ya Umoja wa Mataifa (UN) imesema kuwa majeshi ya upande wa serikali ya Sudan Kusini yameua watu 114 kati ya Julai 2016 na Januari 2017 katika mji wa Yei.
Repoti hiyo ya Kitengo cha Haki za Binadamu cha Shughuli za UN nchini Sudan Kusini (UMNISS) na ofisi ya Haki za Binadamu ya UN imetolewa Ijumaa.
Repoti hiyo pia “inafichua matukio ya wananchi kupigwa mabomu bila ya kutenganisha kuwa sio askari; mauaji yenye kuwalenga; kuibiwa mali zao na kuchomwa kwa mali za raia pamoja na vitendo vya ubakaji vinavyoendeshwa dhidi ya wanawake na wasichana, wakiwemo wale ambao wanakimbia vita.”
UN imesema kuwa makosa haya ya jinai “ yanaweza kufikia kuwa jinai ya kivita dhidi ya binadamu” na kuidhinisha uchunguzi wa kina.
Repoti hiyo imesema kuwa mapigano yamezuka wakati majeshi ya upande wa serikali yalipokuwa yakimsaka mpinzani wa Rais Salva Kiir ambaye aliwahi kuwa naibu wake Riek Machar. “Mapigano hayo yalitokea eneo ambalo alitorokea,” waraka huo umeeleza.
Yei ilikuwa ni “mji wenye amani kwa sehemu kubwa,” UN imesema, ikiwa na wakazi kati ya 200,000 na 300,000 wa makabila tofauti.
Mapigano haya yamesababisha mpasuko mkubwa kati ya makabila na kupelekea watu kulengwa kuuawa, kukamatwa, kubakwa na makundi ya raia kusukumwa nje ya makazi ikakidiriwa kuwa nusu ya watu wanaoishi katika mji huo.
Repoti hiyo inasema kuwa mgogoro wa Yei “ kwa mara nyengine unaonyesha kuwepo kwa mwanya uliosababisha wimbi la uvunjifu wa amani linaloendelea kote nchini Sudan Kusini.
Sudan Kusini imekumbwa na vita vilivyoingia mwaka wan nne tangu mapigano yaanze kati ya zinazo msaidia Kiir na wale wanaompinga Desemba 2013.
UN imesema zaidi ya wananchi milioni 1.8 wa Sudan Kusini wamekimbia nje ya nchi na wengine milioni 1.9 wamepoteza makazi yao kutokana na vita.