Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 16:29

Wakili wa Trump ahukumiwa kifungo cha miaka mitatu


Wakili wa Trump Michael Cohen ( kati ).
Wakili wa Trump Michael Cohen ( kati ).

Michael Cohen, Wakili wa muda mrefu wa Rais wa Marekani Donald Trump amehukumiwa Jumatano kutumikia kifungo cha miaka mitatu baada ya kukutikana na makosa kadhaa.

Mahakama imemkuta na makosa ya uhalifu, ikiwemo kuhusika kwake na mpango wa kufanya malipo ya Dola za Marekani 280,000 ikiwa ni hongo ya kuwanyamazisha wanawake wawili ambao walidai kuwa walikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Trump, na kwa kulidanganya Bunge juu ya juhudi alizokuwa anafanya Trump kujenga nyumba ya ghorofa kubwa Moscow.

Cohen ambaye ana umri wa miaka 52, aliyekuwa akimfanyia kazi zake Trump kwa miaka 12, aliwahi kujigamba kuwa yuko tayari “kupigwa risasi” katika kumsaidia Trump. La ziada hivi karibuni, alisimama dhidi ya kiongozi huyo wa Marekani.

Waendesha mashtaka wamesema Cohen, kwa kumsaidia Trump, alirahisisha kufanya malipo – akivunja sheria za matumizi ya fedha katika kampeni – kwa nyota wacheza filamu za ngono Stormy Daniels na mwanamitindo anayechapishwa katika gazeti la Playboy Karen McDougal muda mfupi kabla ya uchaguzi wa 2016 ili kuwanyamazisha juu ya madai juu ya mahusiano yao na tajiri wa biashara ya majumba miaka kumi kabla ya kugombea kinyang’anyiro cha urais.

Mawakili wa Cohen walikuwa wameomba asitumikie kifungo, wakisema vitendo vyake vilikuwa ni matokeo ya “uaminifu wake wa dhati” kwa Trump..

Wamesema alikuwa na mawasiliano ya karibu na ya kila mara na wafanyakazi wa White House na Wanasheria,” wakati alipokuwa ana andaa kutoa ushahidi katika Bunge mwaka 2017, akidanganya kwa madai ya kuwa Trump alikuwa amesitisha juhudi zake za kujenga Jengo laTrump huko Moscow ilipofika mapema 2016, kabla ya kinyang’anyiro cha ugombea urais wa chama cha Republikan kuanza.

XS
SM
MD
LG