Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 15:57

Trump akaa kimya juu ya hukumu dhidi ya Manafort, Cohen


Trump azungumza na waandishi wa habari baada ya kushuka kutoka katika ndege ya Air Force One Aug. 21, 2018, huko Charleston. W.Virginia.
Trump azungumza na waandishi wa habari baada ya kushuka kutoka katika ndege ya Air Force One Aug. 21, 2018, huko Charleston. W.Virginia.

Rais wa Marekani Donald Trump inawezekana aliwashtua wengi wakati wa mkutano wa kampeni Jumanne usiku wakati alipokaa kimya Jumanne usiku bila ya kutaja hukumu ya kukutikana na makosa iliyotolewa kwa meneja wake wa kampeni wa zamani, Paul Manafort kutokana na tuhuma za kuidanganya benki na kukwepa kulipa kodi mapema siku hiyo huko Virginia.

Kunauwezekano mkubwa kwamba Manafort akatumikia kifungo cha miongo kadhaa.

Akizungumza huko Virginia Magharibi, Trump pia hakutaja jina la wakili wake wa zamani, Michael Cohen, ijapokuwa masaa machache kabla ya hapo Cohen alikubali makosa yake kutokana na mashtaka yaliyoletwa na serikali kuu New York na kukiri alitumia “fedha kuwanyamazisha walamikaji” kwa maelekezo ya Mgombea.

Washirika hao wawili wa Rais Trump wamo hatarini kutumikia vifungo vya muda mrefu jela.

Hata hivyo, Rais Trump amevishutumu vyombo vya habari na wasimamizi wa mashtaka kwa kuendelea kufanya uchunguzi ili kubaini iwapo alishirikiana na Russia katika uchaguzi mkuu wa urais wa mwaka 2016, akisema habari zinazoandikwa na vyombo vy ahabari ni za uongo na kwamba uchunguzi dhidi yake ni hatua ya kumuwinda.

Kabla ya kuwasili kwa mkutano wa kampeni, Rais Trump alisema kwamba anahisi vibaya sana baada ya aliyekuwa meneja wa shughuli zake za Kampeni Paul Manafort kupatikana na hatia lakini akasisitiza kwamba mashtaka hayo hayamhusu.

XS
SM
MD
LG