Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 22:14

Wageni takribani 200 wahudhilia hafla iliyoandaliwa kwa ajili ya rais Yeol


Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol (wa pili kushoto) na mkewe Kim Keon Hee (kushoto), Rais wa Marekani Joe Biden (wa pili kulia) na Mke wa Rais wa Marekani Jill Biden (kulia) wakiwasili katika chakula cha jioni huko, tarehe 26 Aprili 2023. Picha na Brendan SMIALOWSKI / AFP.
Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol (wa pili kushoto) na mkewe Kim Keon Hee (kushoto), Rais wa Marekani Joe Biden (wa pili kulia) na Mke wa Rais wa Marekani Jill Biden (kulia) wakiwasili katika chakula cha jioni huko, tarehe 26 Aprili 2023. Picha na Brendan SMIALOWSKI / AFP.

Muigizaji Angelina Jolie, muandaaji wa kipindi cha Television cha Home Improvement Joanna Gaines mwanariadha wa Olimpiki Chloe Kim walikuwa miongoni mwa orodha ya majina ya watu mashuhuri waliohudhilia hafla iliyoandaliwa na rais Joe Biden kwa ajili ya rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol.

Katika orodha hiyo walikuwepo wageni kuanzia wafanyabiashara, wanasiasa, wanamichezo na burudani walio kuwa wakiburudika. Lea Salonga wa Broadway, alikuwa ni miongoni mwa watumbuizaji wa usiku huo, ambaye alikiri kuwa alipofika hapo alikuwa "amechanganyikiwa" juu ya tukio zima, lililomfanya, "Ahisi kama upo katikati ya hadithi za Abunuasi."

Kwa upande wake Kim, aliongea kwa sauti ya kawaida alipoingia ndani, akiwaambia waandishi wa habari, "Nimesikia chakula kitakuwa kizuri sana." Jolie hakutaka kuzungumza alipowasili akiwa amevalia koti la zamani la Chanel na gauni lenye rangi ya krimu, lakini mwanawe aliyefuatana naye Maddox mwenye umri wa miaka 21, alisema kuwa kitu anachokipenda zaidi kuhusu Seoul ni "watu."

Wanasiasa wachache walikuwepo katika orodha hiyo ya wageni, na wengi wao wakidhamiria kwenye ujumbe, walizungumza mambo mengi sana. Seneta wa Illinois Tammy Duckworth, wa chama cha Demokrat, alisisitiza kuhusu miundo mbinu, upunguzaji wa deni na bajeti. Mwakilishi Judy Chu, Mdemokrat kutoka California, alizungumza kuhusu haki za utoaji mimba. Waziri wa zamani wa Biashara Penny Pritzker, kutoka Illinois ambaye pia ni mfadhili mkubwa wa chama cha Demokrat , alizungumza juu ya mipango ya kongamano la chama cha demokratik litakalofanyika Chicago mwaka 2024, na akiahidi, "bila shaka" litaenda vizuri.

Pia miongoni mwa wageni karibu 200 walikuwepo mwanzilishi mwenza wa Home Depot Arthur Blank; mwandishi wa "Pachinko"Min Jin Lee; na mchezaji wa zamani wa Ligi Kuu ya Baseball, Chan Ho Park. Wengine waliohudhulia ni Seneta Mrepublican Mitt Romney kutoka jimbo la Utah pamoja na magavana wa Delaware, New Jersey na Vermont.

Rais Biden alisema anaamini kuwa ziara ya rais Yoon "itayafanya mataifa hayo mawili kuwa karibu zaidi."

Kwa upande wa Yoon, alitikisa kichwa akiimanisha upendo kulingana na utamadumi wa watu wa Ireland ambako ni asili ya Biden.

"Kuna msemo wa zamani, na Mheshimiwa rais, huyu pia ni muirish, anayesema: Rafiki mzuri ni kama karafuu yenye majani manne, ni vigumu kumpata na bahati kuwa naye," Yoon alisema, na kuongezea "ushirika wetu thabiti”

XS
SM
MD
LG