Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:12

Korea Kusini yakubali kusitisha azma yake ya kutengeneza zana za nyuklia


Kiongozi wa Korea Kusini na Kiongozi wa Marekani wakiandamana na wake zao nje ya White House
Kiongozi wa Korea Kusini na Kiongozi wa Marekani wakiandamana na wake zao nje ya White House

Korea kusini imekubali kutoendeleza mpango wake wa silaha za nyuklia ikiwa ni sehemu ya kurudisha nafasi kubwa ya kufanya maamuzi katika mpango wa dharura ya Marekani katika tukio la shambulio la nyuklia la korea kaskazini.

Marekani na korea kusini zimetangaza makubaliano leo wakati rais wa korea kusini Yoon Suk Yeol akiwa katika ziara ya kikazi white house kusherehekea miaka 70 ya uhusiano wa pande mbili na kujadiliana na mwelekeo wa baadaye wa ushirikiano wa nchi hizo.

Tangazo la Washington ni matokeo ya mfululizo wa mambo kadhaa yaliyojadiliwa miezi mingi na ahadi za Marekani za kuzuia jamhuri ya korea Kaskazini kuendeleza program ya silaha za nyuklia, afisa wa juu wa utawala alisema jana jioni wakati akiongea na waandishi wa habari.

Chini ya mpango huo maafisa wamesema seol itadumisha hadhi yake isiyo ya Nyuklia na itaendelea kutii masharti yote ya kutia saini mkataba wa kuzuia kueneza silaha za maangamizi. Mkataba wa NPT na korea ulipitishwa mwaka 1975 na kuzuiya pande zote kutengeneza silaha za nyuklia.

Nchi hizo mbili pia zitaunda kundi la mashauriano ya nyuklia- NCG , utaratibu wa mara kwa mara wa mashauriano kati ya nchi mbili ambao utazingatia maswala ya nyuklia na mipango ya kimkakati na utawapa washirika wetu wa ROK ufahamu wa ziada wa jinsi tunavyofikiri kuhusu kupanga wakati wa dharura,” afisa huyo aliongeza kusema.

Zaidi ya kushirikiana habari zaidi, seoul itakuwa na sauti kubwa katika mijadala ya kupeleka sialaha za Marekani .

XS
SM
MD
LG