Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:10

Joe Biden kuwania tena urais 2024


Rais wa Marekani Joe Biden akisalimiana na mashabiki wakati wa ufunguzi wa Michezo ya Maccabiah huko Jerusalem, tarehe 14 Julai 2022. Picha na RONEN ZVULUN / POOL / AFP.
Rais wa Marekani Joe Biden akisalimiana na mashabiki wakati wa ufunguzi wa Michezo ya Maccabiah huko Jerusalem, tarehe 14 Julai 2022. Picha na RONEN ZVULUN / POOL / AFP.

Rais wa Marekani Joe Biden alizindua rasmi kampeni yake ya kuwania tena urais siku ya Jumanne, katika ujumbe wa video, Biden aliwaomba wapiga kura wampe muda zaidi wa "kumaliza kazi" utawala wake iliyoianza miaka miwili iliyopita.

Wagombea rasmi kutoka vyama viwili vikuu vya siasa nchini Marekani, Demokrat na Republican, hawata chaguliwa kwa zaidi ya mwaka mmoja, miezi kadhaa kabla ya uchaguzi wa Novemba 2024.

Lakini kuwepo kwa Biden madarakani kunamaanisha itakuwa vigumu kwa mfano ukizingatia kwamba wafuasi wa chama cha Demokratic kumchagua mtu mwingine kama mgombea wao. Biden alimshinda rais kutoka chama cha Republican Donald Trump katika uchaguzi wa mwaka 2020 na kuchukua madaraka ya muhula wake wa kwanza.

Trump alikataa kukubali matokeo ya uchaguzi, akitoa madai yasiyo na msingi ya wizi katika uchaguzi. Umati wa wafuasi wa Trump walivamia jengo la bunge la Marekani wakati wabunge walipokuwa wakikutana ili kurasmisha uchaguzi hapo Januari 2021, na kampeni ya Biden zilitumia matukio ya shambulio hilo kutangaza azma yake siku ya Jumanne.

"Kila kizazi cha Wamarekani kimekabiliwa na wakati ambapo wanapaswa kutetea demokrasia," Biden alisema. "Msimame kwa uhuru wetu wenyewe. Msimame kwa haki ya kupiga kura na haki zetu za kiraia.”

Aliwataja warepublican kuwa wanafanya kazi ya kuzuia fursa ya utoaji mimba, kupunguza fedha kwa ajili ya Usalama wa Jamii, kuweka vizuizi kwa haki za kupiga kura na "kuwaambia watu, nani wanaweza kumpenda."

Biden, ambaye alikuwa rais mwenye umri mkubwa zaidi wa taifa hili wakati wa kuapishwa kwake, amepuuza wasiwasi kuhusu umri wake kabla ya kampeni nyingine ya urais. Atakuwa na umri wa miaka 82 atakapoanza muhula mpya wa uraisi.

Biden ameweka matarajio yake katika mafanikio yake ya kiutawala katika muhula wa kwanza na uzoefu wa zaidi ya miaka 50 Washington ambao utakuwa muhimu zaidi kuliko wasiwasi juu ya umri wake.

Anakabiliwa na njia nyepesi ya kushinda uteuzi wa chama chake, bila wapinzani wakubwa wa Demokrat. Lakini anatrajiwa kuwa tayari kwa mapambano makali ya kushikilia nafasi hiyo ya urais katika taifa lililogawanyika sana.

Baadhi ya habari hizi zinatoka katika Shirika la habari ka AP

XS
SM
MD
LG