Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:08
VOA Direct Packages

Marekani haitavuja uhusiano wa kibiashara na China


Maonyesho ya kibiashara ya China. Picha ya maktaba
Maonyesho ya kibiashara ya China. Picha ya maktaba

Mwakalishi wa biashara wa Marekani Katherine Tai amesema Alhamisi wakati akiwa mjini Tokyo kwamba Washington haina nia ya kuondoa uchumi wake kutoka China.

Tai yupo kwenye ziara yake ya nne nchini Japan tangu alipochaguliwa kama mwakilishi mkuu wa biashara wa Marekani, na amesema kwamba maafisa wote wa utawala wa Rais Joe Biden wameeleza bayana kwamba hawana nia ya kujitenga na uchumi wa China, akiongeza kwamba vikwazo vya kibiashara vya Marekani dhidi ya taifa hilo vinalenga watu wachache tu.

Wakati akizungumza na wanahabari, Tai amesema kwamba kutokana na umuhimu na ukubwa wa uchumi wa China, suala la Marekani kujitenga nao haliwezi kufikiwa. Baadhi ya maafisa wa China wamekuwa wakilalamikia vikwazo vya kiuchumi vya Marekani, pamoja na kanuni nyingine za kushirikiana teknolojia na China, wakidai kuwa Washington inajaribu kudhibiti taifa hilo dhidi ya kuimarika zaidi kiuchumi.

Tai amesema kwamba licha ya kuwa hana nia ya kutembelea China hivi karibuni, biashara za kawaida kati ya Marekani na China zingali zinaendelea, na kwamba wapo tayari kuendelea kushauriana na wenzao wa Beijing.

XS
SM
MD
LG