Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 19:56

Waasi wa Hayat Tahrir al-Sham waiteka miji miwili iliyokuwa chini ya serikali


Jengo linatoa moshi huko katika mkoa wa Homs. Ndege za Russia zilifanya mashambulizi ya angani katika mikoa mitatu ya Syria ikiwemo kwa mujibu wa vyombo vya usalama vya Syrian, Sept. 30, 2015.
Jengo linatoa moshi huko katika mkoa wa Homs. Ndege za Russia zilifanya mashambulizi ya angani katika mikoa mitatu ya Syria ikiwemo kwa mujibu wa vyombo vya usalama vya Syrian, Sept. 30, 2015.

Waasi wa kikundi cha Hayat Tahrir al-Sham (HTS) wamesema walikuwa wameikamata miji ya Syria ya Talbis na Rastan.

Hatua hiyo imewafikisha ndani ya kilometa kadhaa karibu na mji wa Homs, kanda za video katika mitandao ya kijamii Ijumaa (Desemba 6) zinaonyesha kile kilichosemwa ni waasi wakipita na magari katika mji wa Rastan.

Kanda ya video hiyo iliyochukuliwa kutoka juu ya jengo moja, iliwaonyesha wapiganaji hao wakipita na magari na pikipiki wakifyatua risasi hewani kusherehekea wakati msafara huo ulipopita mjini humo.

Shirika la Habari la Reuters liliweza kuthibitisha eneo hilo kuwa ni Rastan, mji ulioko takriban kilomita 20 kaskazini mwa Homs, kutokana na mpangilio wa mitaa, majengo, mnara wa msikiti na mnara wa saa unaonekana kutoka mbali unaofanana na picha za satalaiti na picha za kumbukumbu.

Reuters haikuweza kuthibitisha tarehe maalum video hiyo ilichukuliwa, lakini Kikundi kinachofuatilia haki za binadamu Syria kimeripoti kuwa mji huo ulichukuliwa na waasi Ijumaa (Desemba 6).

Mashambulizi ya mabomu yaliyofanywa na Russia usiku kucha yameharibu daraja la Rastan katika barabara kuu ya M5, ambayo ndiyo njia kuu kwenda Homs, kuwazuia waasi hao kulitumia kusonga mbele, afisa wa jeshi wa Syria ameiambia Reuters.

Hezbollah imetuma idadi ndogo ya “vikosi vya uangalizi” kutoka Lebanon kwenda Syria usiku kucha kuwasaidia kuzuia waasi wanaipinga serikali kuukamata mji wa kimkakati wa Homs, maafisa wawili wa ngazi ya juu w wa Lebanon wameiambia Reuters.

Afisa wa jeshi la Syria na maafisa wawili wa kanda ambao wako karibu na Tehran pia wameiambia Reuters kuwa vikosi maalum kutoka kikundi kinachoungwa mkono na Iran, Hezbollah walivuka kutoka Lebanon na kuingia Syria usiku kucha na wameanza ulinzi wa Homs.

Forum

XS
SM
MD
LG