Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 17:46

Waandishi wawili wauawa na genge lenye silaha nje ya Port-Au-Prince


Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry (REUTERS/Ralph Tedy Erol/File Photo)
Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry (REUTERS/Ralph Tedy Erol/File Photo)

Waaandishi wa habari wawili raia wa haiti wameuawa karibu na mji wa Port-au-Prince nchini humo baada ya washukiwa wa genge lenye silaha kuwafyatulia risasi kundi la waandishi wa habari waliowasili eneo hilo kumhoji kiongozi wa genge hasimu.

Kulingana na polisi na ripoti za vyombo vya habari nchini humo, waandishi waliouawa ni Amady John Wesley, mwandishi wa kituo cha radio cha Ecuote FM cha Montreal, na Wilguens Louissaint.

Kituo cha radio cha Ecoute kimethibitisha kifo cha mwandishi wao na kusema mauaji hayo kuwa ni uhalifu na tukio la kinyama.

Polisi wamesema kwamba mwandishi wa tatu alinusurika katika shambulizi hilo.

Magenge kadhaa yenye silaja yanapigania kudhibiti sehemu ya Laboule 12, ambapo mauaji hayo yalitokea.

XS
SM
MD
LG