Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 08, 2024 Local time: 09:14

Waandamanaji Uganda wamefunguliwa mashtaka ya uzururaji


Mwandamanaji akikamatwa jijini Kampala, Uganda
Mwandamanaji akikamatwa jijini Kampala, Uganda

Vijana 42 wamefikishwa mahakamani na kuamrishwa kuzuiliwa gerezani nchini Uganda baada ya kufunguliwa mashtaka ya kushiriki maandamano yaliyopigwa marufuku na serikali, jana Jumanne.

Waandamanaji walijitokeza mjini Kampala Jumanne wakuwa wamebeba mabango na kupaaza sauti zenye kupinga ufisadi bungeni.

Wakili Benard Oundo, ambaye ni rais wa muungano wa mawakili Uganda, na anayeongoza kundi la mawaikili wanaowakilisha vijana waliokamatwa, amesema kwamba walifikishwa mahakamani Jumanne jioni, na kufunguliwa mashtaka mbalimbali yakiwemo kuzurura bila kuwa na shughuli maalum, pamoja na kuwa kero kwa uma.

Washukiwa wamepinga mashtaka dhidi yao, na wameamurishwa kurudi mahakamani kati ya tarehe 30 July na Agosti 6.

Shirika la Human rights watch, lenye makao yako makuu mjini New York, limesema kwamba kukamatwa kwa waandamanaji ni dhihirisho kwamba serikali ya rais Yoweri Museveni haiheshimu haki ya watu kuandamana na kujieleza.

Viongozi wa upinzani na watetezi wa haki za kibinadamu wamesema kwamba ufisadi na ubadirifu wa mali ya uma umekithiri nchini Uganda na kwamba rais Museveni ameshindwa kuchukua hatua dhidi ya maafisa wa ngazi ya juu katika serikali yake ambao ni mafisadi kwa sababu ni watu wake wa karibu.

Forum

XS
SM
MD
LG