Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:57

Kampuni ya Ufaransa inaendelea na mradi wa kuchimba visima nchini Uganda licha ya upinzani wa wanamazingira


Mwonekano wa jumla wa kisima cha TotalEnergies kinachojengwa ndani ya Mbuga ya Kitaifa ya Murchison Falls magharibi mwa Uganda Februari 22, 2023.
Mwonekano wa jumla wa kisima cha TotalEnergies kinachojengwa ndani ya Mbuga ya Kitaifa ya Murchison Falls magharibi mwa Uganda Februari 22, 2023.

Uzalishaji bado haujaanza, lakini mradi wa mafuta wenye utata wa TotalEnergies huko Afrika Mashariki tayari unaathiri vibaya mazingira katika mbuga kubwa za kitaifa nchini Uganda shirika la hifadhi lilisema  Ijumaa.

Licha ya upinzani kutoka kwa wanamazingira na wanaharakati wa haki, kampuni kubwa ya nishati ya Ufaransa inaendelea na mradi wake wa kuchimba visima wa Tilenga nchini Uganda na bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) lenye urefu wa kilomita 1,443 ili kusafirisha mafuta yake hadi pwani ya Tanzania.

Mradi huo wenye thamani ya dola bilioni 10 unahusisha uchimbaji wa visima zaidi ya 400 vya mafuta magharibi mwa Uganda, vingi vikiwa katika hifadhi ya taifa ya Murchison Falls, ambako kuna viumbe hai na mbuga kubwa zaidi ya kitaifa nchini humo.

Forum

XS
SM
MD
LG