Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 13:25

Vita vyaendelea Gaza wakati sitisho la mapigano likisubiriwa

Moshi ukifuka baada ya mashambulizi ya Israel Kaskazini mwa Gaza Novemba 23, 2023.Picha na John MACDOUGALL / AFP.
Moshi ukifuka baada ya mashambulizi ya Israel Kaskazini mwa Gaza Novemba 23, 2023.Picha na John MACDOUGALL / AFP.

Vita vinaendelea huko Gaza hivi Alhamisi wakati pendekezo la sitisho la mapigano na kuachiliwa kwa mateka limecheleweshwa kwa siku moja zaidi.

Vita vinaendelea huko Gaza hivi Alhamisi wakati pendekezo la sitisho la mapigano na kuachiliwa kwa mateka limecheleweshwa kwa siku moja zaidi.

Moshi mweusi umeonekana umetanda angani kaskazini mwa Gaza kwenye eneo la vita kote katika uzio wa Israel wakati wa asubuhi katika ukanda huo. Israel imesema kuachiliwa kwa mateka kunatakiwa kuambatane na sitisho la kwanza la vita, linawezakucheleweshwa hadi ijumaa.

Jeshi la Israel limesema limefanya mashambulizi ya anga 300 hapo jana, na kupiga ving’ora kuonya kuhusu kurushwa kwa roketi kuvuka mpaka kunakofanywa na makundi ya kipalestina yenye silaha.

Vyombo vya habari vya Palestina vimeripoti mashambulizi ya Israel maeneo ya kaskazini pamoja na mji wa kusini wa Khan Younis ambako Israel imewaambia wakazi wa kaskazini kutafuta hifadhi.

Mshauri wa usalama wa taifa wa Israel Tzachi Hanegbi alisema katika taarifa kwamba “mashauriano ya kuachiliwa kwa mateka yanaendelea taratibu.

Forum

XS
SM
MD
LG