Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 13:34

Qatar kutoa tangazo kuhusu kuanza sitisho la  mapigano na kuachiliwa kwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas

Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar Mohammed bin Abdulrahman Al Thani, katikati, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, kushoto, wakihudhuria mkutano, mjini Doha, Qatar, Ijumaa Oktoba 13, 2023.

Qatar ilisema Alhamisi tangazo kuhusu kuanza kwa sitisho la  mapigano kati ya Israel na Hamas na kuachiliwa kwa mateka na wafungwa linaweza kufanyika  baadaye alhamisi, baada ya kucheleweshwa kwa utekelezaji wa makubaliano ambayo pia ilimaanisha kusaidia misaada ya kibinadamu kufika Ukanda wa Gaza.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar Majed Al-Ansari alisema, Makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa yatakamilishwa katika saa zijazo.

Mshauri wa usalama wa taifa wa Israel, Tzachi Hanegbi, alisema katika taarifa yake Jumatano jioni kwamba mazungumzo yanaendelea na kwamba mateka wa kwanza wanaoshikiliwa na Hamas huko Gaza hawataachiliwa mpaka Ijumaa.

Forum

XS
SM
MD
LG