Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 02, 2025 Local time: 23:20

Viongozi wa kidini wakusanyika Paris kuonyesha ushirikiano kwenye Olimpiki


Baadhi ya viongozi wa kidini wakiwa karibu ba hema ya wanariadha wa Olimpiki mjini Paris.
Baadhi ya viongozi wa kidini wakiwa karibu ba hema ya wanariadha wa Olimpiki mjini Paris.

Viongozi wa kidini pamoja na maafisa wa Olimpiki Jumapili wamekusanyika nje ya hekalu la Notre Dame mjini Paris, kuonyesha namna dini na spoti zinavyoweza kushirikiana, kulingana na mkuu wa Kamati ya Olimpiki Thomas Bach.

Michezo ya Olimpiki mwaka huu nchini Paris ilifunguliwa wakati ikizua utata mkubwa miongoni mwa makundi ya kidini ikiwemo Vatican. Mengi ya makundi hayo yalilalamikia kile walichosema kuwa kenjeli ya chakula cha mwisho cha Yesu na watumishi wake, ingawa waandaji wamepinga madai hayo wakisema kuwa ufunguzi huo uliendana na picha iliochorwa na Leonardo da Vinci.

Kando na utata huo, kuna hema lililotengenezwa karibu na kijiji cha wanariadha mjini Paris, ambapo viongozi wa kidini kutoka dini 5 kubwa ulimwenguni wanatoa huduma za kiroho kwa wanariadha wanaoshirikia michezo hiyo.

Wawakilishi wa dini za Budhaa, Hindi, Kikiristo, Kiislamu na Kiyuda walitumia miezi kadhaa kuunda eneo hilo, ambapo zaidi ya wanariadha 10,500 pamoja na wasaidi wao wanaweza kupata msaada wa Imani, pamoja na kuabudu.

Forum

XS
SM
MD
LG