Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 23:08

Vikosi vya Israeli vyashambulia maeneo kadhaa ya Gaza


Wapalestina wakagua eneo liloshambuliwa na vikosi vya Israeli.
Wapalestina wakagua eneo liloshambuliwa na vikosi vya Israeli.

Vikosi vya Israel siku ya Ijumaa vilishambulia maeneo ya Ukanda wa Gaza, huku mashahidi wakiripoti uvamizi wa angani kuzunguka mji wa kusini wa Rafah, eneo ambalo limekuwa likiangaziwa  zaidi katika vita vya karibu miezi minane.


Israel ilianzisha uvamizi wake wa kijeshi katika mji wa Rafah mapema mwezi Mei licha ya pingamizi za kimataifa kuhusu usalama wa raia wanaoendelea kupata hifadhi katika mji huo kwenye mpaka wa Gaza na Misri.


Shambulizi lililoua watu kadhaa katika kambi ya watu waliokimbia makazi yao mwishoni mwa juma ulizua wimbi la shutuma mpya.


Walioshuhudia walisema Ijumaa kuwa mashambulizi ya Israel yalipiga eneo la Rafah pamoja na Nuseirat katikati mwa Gaza, na mwandishi wa AFP aliripoti mashambulizi makali ya mabomu kaskazini mwa Gaza.


Mashambulizi katika maeneo mawili tofauti yalisababisha vifo vya watu 11 kwa usiku mmoja, vyanzo katika hospitali ya Deir al-Balah na kambi ya wakimbizi ya Nuseirat vimeripoti.

Forum

XS
SM
MD
LG