Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 15:03

Ndege nyingine ya Marekani ya MQ-9 imeanguka nchini Yemen


Mfano wa ndege aina ya MQ-9 ya Marekani iliyoanguka nchini Yemen. Jan. 23, 2018.
Mfano wa ndege aina ya MQ-9 ya Marekani iliyoanguka nchini Yemen. Jan. 23, 2018.

Picha zilizoelezewa na AP zilionyesha MQ-9 imeanguka katika jangwa na eneo lake la mkia limekatika kutoka kichwa cha ndege.

Ndege nyingine ya Marekani aina ya MQ-9 Reaper isiyokuwa na rubani, ilianguka nchini Yemen, picha zilionyeshwa Jumatano, wakati waasi wa ki-Houthi nchini Yemen wakiendelea na mashambulizi ya meli katika bahari ya Sham kutokana na vita vinavyoendelea vya Israel na Hamas.

Wa-houthi walitoa kanda ya video ambayo walisema ilionyesha ndege hiyo ikilengwa na kombora kutoka ardhini kwenda angani katika eneo la jangwa kwenye mkoa wa kati wa Marib nchini Yemen. Hii ni mara ya tatu kwa tukio hilo kufanyika mwezi huu pekee.

Picha zilizoelezewa na shirika la habari la Associated Press zilionyesha MQ-9 imeanguka katika jangwa hilo, eneo lake la mkia limekatika kutoka kichwa cha ndege. Angalau mlango moja wa dharura kwenye drone hiyo ulionekana kufunguliwa baada ya kutua, ingawa drone ilibakia kwa sehemu kubwa bila uharibifu wowote uliowekwa wazi kuhusu mlipuko.

Picha moja ilionyesha tarehe ya Jumatano. Drone hiyo haikuonekana kuwa na alama zozote.

Forum

XS
SM
MD
LG