Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 19:49

Utoaji mimba usio salama wachangia ongezeko la vifo kwa wajawazito Kenya


Sanamu la msichana mjamzito lililoko Nairobi, Mchongaji wa sanamu hilo Jens Galschiot, alisema ni upinzani dhidi ya msimamo wa Kanisa Katoliki linalopinga uzazi wa mpango. Picha na Reuter/ Antony Njuguna.
Sanamu la msichana mjamzito lililoko Nairobi, Mchongaji wa sanamu hilo Jens Galschiot, alisema ni upinzani dhidi ya msimamo wa Kanisa Katoliki linalopinga uzazi wa mpango. Picha na Reuter/ Antony Njuguna.

Utoaji mimba umezuiliwa nchni Kenya, lakini katika Kaunti ya Kilifi upande kusini mwa pwani ya nchi hiyo, wanawake wengi na wasichana wanaopata uja uzito bila ya kupanga wanasema hawana uchaguzi isipokuwa kupitia utoaji mimba hatari bila ya msada wa muuguzu au daktari.

Wanaharakati wa ndani wanasema utaratibu huu unachangia viwango vya juu mno vya vifo kwa wajawazito katika eneo hilo.

Mercy katan ambaye ni mwanafunzi anasema alipata uja uzito wakati alipokuwa bado yuko shule ya sekondari. Amesema mpenzi wake alikataa kumsaidia na wazazi wake walimkataa, kwa hiyo hakuna na njia nyingine isipokuwa kwenda kuitoa mimba hiyo bila ya msaada wa mtalaamu wa afya.

Madaktari wa afya kama Mwanakarama Athman Mohamed ambaye ni muuguzi anayetoa huduma za uzazi wa mpango amesema Mercy ana bahati. Si wanawake wote ambao wanapitia utoaji mimba usio salama wanafika hata hospitali.

“Unampata mtu ambaye huenda mfuko wake wa uzazi umeoza, naunweza kupata hali ya Septicaemia. Septicaemia ni hali mbaya sana ya maambukizi na mara nyingi yanaingia katika mfumo wa damu, na kusambaa katika mwili hadi kwenye ubongo. Ndiyo maana hivi sasa tunapata vifo,” amesema.

Mwanafunzi wa shule ya sekondari Jackline Bosibori akiwa mjamzito huko Kibera.
Mwanafunzi wa shule ya sekondari Jackline Bosibori akiwa mjamzito huko Kibera.

Utoaji mimba ni kinyume cha sheria nchini kenya, labda afya ya mama iwe katika hatari. Lakini madaktari wanakadiria kwamba karibu mimba nusu milioni zinatolewa kila mwaka nchini kenya, nyingi ya mimba hizo hutolewa ka njia isiyo salama.

Leila Abdulkheir Isaak ni afisa mtendaji mkuu katika Youth Voices and Action Initiative, kundi la kutetea afya ya uzazi kwa wanawake. Anasema kuna hadithi nyingi kama ya Katana na anasema kundi hilo linataka kuwasaidia vijana wa kike kukabiliana na mimba ambazo hazikupangwa kufanya maamuzi mazuri.

“Wanawake na wasichana, wengi wao hawana habari kuhudu afya ya uzazi…. Pia tunawapatia habari kuhusu matatizo ya utoaji mimba, baada ya kutoa mimba, huduma za utoaji mimba, na masuala ya haki za wagonjwa katika misingi ya fursa ya huduma za afya ya uzazi,” amesema afisa mtendaji mkuu huyo wa kundi la kutetea afya ya uzazi kwa wanawake.

Josephine Wanjiru akiwa darasani katika shule ya sekondari ya Serene Haven inayotoa mafunzo kwa wasichana wajawazito huko Nyeri
Josephine Wanjiru akiwa darasani katika shule ya sekondari ya Serene Haven inayotoa mafunzo kwa wasichana wajawazito huko Nyeri

Kundi hilo lilimpatia mafunzo mfanyakazi wa kujitolea Emily Nasubo kuzungumza na wateja kuhusu afya ya uzazi. Anasema hadithi za kusikitisha za wanawake na wasichana waliopitia maumivu ya utoaji mimba zimemhamasisha kuunga mkono juhudi hizi.

Katika muda wa miezi sita iliyopita, Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Kilifi imerekodi takriban kesi 500 za matibabu baada ya utoaji mimba.

Kennedy Miriti mratibu wa program ya afya ya uzazi katika hospitali hiyo, anasema kiwango cha vifo miongoni mwa wanawake wajazito nchini Kenya kiko juu mno.

“Pia tunafuatilia kufahamu nini sababu za vifo vya wajawazito ambazo hatujazitambua na zinasababisha vifo vyote hivyo. Kwa kweli utoaji mimba ni moja ya sababu hizo,” amesema Miriti.

Madaktari wanakdiria kwamba kiasi cha wanawake saba na wasichana wanafariki kila siku kutokana na utoaji mimba usio salama na maelfu wanalazwa hospitali.

Forum

XS
SM
MD
LG