Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 18:53

Mwanamke aliyejitoa mhanga kupambana dhidi ya wanawake Kenya


Wanawake wakishiriki kwenye maandamano ya kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani huko Nairobi Machi 8, 2022. Picha na Yasuyoshi CHIBA / AFP
Wanawake wakishiriki kwenye maandamano ya kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani huko Nairobi Machi 8, 2022. Picha na Yasuyoshi CHIBA / AFP

Ukatili wa kijinsia bado ni tatizo la kijamii na ukiukaji wa haki za kibinadamu, ambao unaathiri sana wanawake kuliko wanaume duniani. Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha mwanamke mmoja kati ya watatu duniani wanapitia dhuluma za kijinsia za aina moja au nyingine.

Katika kufuatilia visa hivi, mwanamke mmoja nchini kenya Betty Sharon, amekuwa mstari wa mbele kupambana na ukatili wa kijinsia ambao umekua changamoto kubwa kwa wanawake.

Sharon mwenye umri wa miaka 53, na mama wa watoto wawili. Alianza harakati za kutetea haki za wanawake na watoto miaka 20 iliyopita, kwa lengo la kupaza sauti za wanyonge dhidi ukatili wa kijinsia.

Mtetezi huyo ambae alisomea taaluma ya famasia, Aliungana na wanawake wenzake na kuanzisha shirika la Collaboration for Women in Development, mwanzoni lilijulikana kama COAS Women in Development mwaka 2005.

Sharon anieleza kuwa dhuluma alizopitia katika ndoa yake, pamoja marafiki zake walimpa msukumo wa kutetea haki za wanawake wenzake wanaopitia dhuluma za aina hiyo.

“Wakati huo kulikua na visa vingi vya dhuluma za ngono hasa kwa watoto wa kike kutoka kwa watalii waliokua wakizuru pwani ya Kenya,” alisema Sharon.

Kupitia shirika hilo Sharon na wanawake wenzake wamekuwa wakitumia michezo kama soka, sanaa na hata mazungumzo kueneza hamasa kuhusu uongozi, na haki kwa wanawake na watoto.

Mbali na kuzungumza tu na jinsia ya kike, alianzisha mradi wa badilika, ambao ulinuia kuwabadilisha wanaume waliofungwa kutokana kesi za dhuluma za ngono katika gereza la shimo la Tewa, Mombasa.

Ikifahamika kuwa wanaume ndio washukiwa wakuu wa unyanyasaji wa kijinsia, aliwafunza kuhusu afya ya uzazi na umuhimu wa kumhusisha mwanamke katika maamuzi.

Shughuli za utetezi zinataka kisomo cha maswala ya jamii na maendeleo na pia sheria. Sharon akariri kuwa mbali na kuwelimisha wengine, yeye binafsi hajutii kujiunga na utetezi kwa kuwa umemsaidia kusoma zaidi, maswala ya sheria, afya ya uzazi na mengineyo katika kupinga ukatili wa kijinsia.

Ingawa bado kenya inaripoti visa vya dhulma za kijinsia hasa ukatili wa mauaji ya kiholela miongoni mwa wanawake, Sharon asema watetezi wamepiga hatua kubwa huku Mombasa ikiwa pamoja na mahakama ya kusikiza kesi za dhulma za kijinsia wakati vituo vya polisi wakiweka meza ya kupokea mashitaka ya waadhirika.

Kutokana na juhudi zake, ametuzwa humu nchini na kimataifa, huku shirika lake la Collaboration for Women in Development, kwa miaka miwili kwa kuwa shirika bora lisilo la serikali Afrika katika maswala ya uongozi.

Amewakilisha watetezi wa kenya katika makongamano mbali mbali, na pia ni wenyekiti wa kitengo cha afya katika muungano wa mashirka yasio ya serikali katika eneo la pwani ya Kenya.

Akizungumzia changamoto za kazi yake Sharon alisema kuwa mbali na tuzo alizopata, lakini amekuwa akikumbwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za kutishiwa maisha yake na hata kuvunjiwa ofisi.

Forum

XS
SM
MD
LG