Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 06:18

Usomaji wa magazeti Sudan umeshuka


Mkaazi wa Sudan akisoma gazeti la Juba Monitor. Agosti 21, 2015 mjini Juba.
Mkaazi wa Sudan akisoma gazeti la Juba Monitor. Agosti 21, 2015 mjini Juba.

Magazeti katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki yamekumbwa na miaka kadhaa ya udhibiti wa kisiasa na hali ngumu ya uchumi.

Kadri mzozo wa uchumi unavyozidi kuongezeka na ndivyo wasomaji wanavyozidi kushikamana na simu zao, sekta ya magazeti iliyokuwa imeshamiri nchini Sudan kwa sasa imeshuka, wakati wachapishaji wa magazeti wanafunga au kupunguza shughuli zao za uchapishaji , uuzaji, uhariri, maafisa ya vyama vya wafanyakazi wameliambia Shirika la habari la Reuters.

Magazeti katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki yamekumbwa na miaka kadhaa ya udhibiti wa kisiasa na hali ngumu ya uchumi. Kwa kiasi kikubwa hivi sasa wananchi wanapata habari kwenye mitandao, wakati mwingine kutoka kwenye magazeti kwa njia ya mtandao, lakini pia kupitia mitandao ya kijamii, ambako uvumi na habari potofu zimeenea.

“Uandishi wa habari wa magazeti unakalibiwa na changamoto zilizopo” alisema Mohamed Abdelaziz ambaye ni katibu mkuu wa Umoja wa Waandishi wa Habari wa Sudan, muungano ulioanzishwa kwa mara nyingine tena mwaka jana.

Abdelaziz amesema kuna upungufu mkubwa wa idadi na kiwango cha magazeti ambayo yanaendelea kuchapishwa, hadi kufikia asilimia zaidi ya tisini. Abdelaziz alisema, hali ambayo imesababishwa na waandishi wengi wa magazeti wameacha au kuachishwa kazi.

“Ninapendelea uandishi wa habari wa magazeti, natumaini hautakufa, kwa sababu jamii yetu inahitaji uaminifu unaotoa” amesema Youssef Hamad, mhariri mkuu wa gazeti la Al-Hadatha, ambalo kwa sasa kutokana na sababu za kiuchumi na kisiasa gazeti hilo linachapishwa mtandaoni. Aliongeza kuwa upungufu wa usambazaji wa magazeti nje ya mji mkuu wa Khartoum umeongezeka.

Chanzo cha habari hii kinatoka shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG