Kimbunga Chido kilichopiga Msumbiji siku ya Jumapili kimesababisha vifo na uharibifu wa majengo na miundombinu.
Amegusia matokeo ya muda mrefu ni pamoja na watoto kukatishwa masomo na kuenea kwa magonjwa ya maambukizo yatokanayo na maji machafu, kwa sababu ya watu kushindwa kufikia huduma za afya.
Mkuu wa mashauriano na mawasiliano wa UNICEF Msumbiji, Taylor ameeleza haya:
“ UNICEF ina wasiwasi kuhusu matokeo ya haraka yakimbunga . vifo vilivyotokea, uharibifu wa shule hadi nyumba za watu, hadi kwenye majengo ya huduma za afya.
Tuna wasiwasi pia kuhusu matokeo ya muda mrefu. Watoto wamekatishwa masomo kwa wiki kadhaa. Watu wameshindwa kufikia huduma za afya na kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza yatokanato na maji machafu kama vile kipindupindu na Malaria.”
Forum