Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 20:20

Ukraine yasema inaimarisha ulinzi wa anga, itajibu mashambulizi ya Russia


Rais wa Russia Vladimir Putin
Rais wa Russia Vladimir Putin

Waziri wa ulinzi wa Ukraine Rustem Umerov amesema serikali yake ilikuwa inaongeza uwezo wa ulinzi wa anga.

Ameyasema hayo wakati akijibu kuhusu mashambulizi ya makombora ya masafa marefu yaliyofanywa na Russia katika mji wa ukarine wa Dnipro.

Umerov alitoa ufafanuzi huo leo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari akiwa na mwenzake wa Sweden Pal Johnson huko mjini Stockholm, Sweden.

Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Rustem Umerov na mwenzake wa Sweden Pal Jonson wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari, Stockholm, Sweden Novemba 22, 2024. TT News Agency/Jessica Gow via REUTERS
Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Rustem Umerov na mwenzake wa Sweden Pal Jonson wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari, Stockholm, Sweden Novemba 22, 2024. TT News Agency/Jessica Gow via REUTERS

Jonson ameongeza kuwa shambulizi la Russia haliwezi kuikatisha tamaa nchi yake katika uungaji mkono wa serikali yake kwa Ukraine.

Alhamisi Russia ilifyatua makombora ya masafa marefu kujibu hatua ya Marekani na Uingereza kuiruhusu Kyiv kushambulia ndani ya ardhi ya Russia na silaha zake za Magharibi za ubora wa juu.

Forum

XS
SM
MD
LG