Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 07:20

Ukraine, NATO zatofautiana juu ya uhakika wa Russia kufanya shambulizi


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akiongea kwa njia ya simu na Rais wa Marekani Joe Biden.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akiongea kwa njia ya simu na Rais wa Marekani Joe Biden.

Kiongozi wa Ukraine na washauri wake wa ulinzi na usalama wanatathmini azma za kiongozi wa Russia Vladimir Putin kwa njia tofauti ikilinganishwa na wenzao wengi wa Magharibi.

Je, wana uvumilivu zaidi baada ya miaka minane ya uchokozi ulioendelea wa Russia na vita vya muda mrefu huko mashariki mwa Ukraine – au hawajamuelewa vizuri adui yao Russia?

Washington na London wote wameonya juu ya uwezekano mkubwa kwamba Putin ataamuru uvamizi wa Ukraine. Rais wa Marekani Joe Biden amekuwa akitahadharisha kwa wiki kadhaa kuhusu “uwezekano wa kipekee” Russia huenda ikaivamia Ukraine mwezi ujao, na kusisitiza hilo Alhamisi katika mazungumzo ya simu na rais wa Ukraine Volocymyr Zelenskiy, kwa mujibu wa White House.

Waziri wa Ulinzi wa Uingereza, Ben Wallace, anasema yeye “hana matumaini” kuwa uvamizi wa Russia huko Ukraine unaweza kuzuilika. Ameiambia BBC wakati akiitembelea Berlin kuwa bado kuna “nafasi” kwamba uvamizi huo unaweza kusitishwa, lakini akaongeza, “mimi sina matumaini.”

Ben Wallace
Ben Wallace

Russia imekanusha kuwa inajiandaa kufanya shambulizi kubwa dhidi ya Ukraine, ikiyashutumu mataifa ya Magharibi wa kuleta hofu. Kremlin inasisitiza kuwa wanajeshi zaidi ya 100,000 walipelekwa kwenye mpaka na Ukraine kama sehemu ya mazoezi ya kijeshi.

Lakini Zelenskiy anaonekana kuishuku Moscow itafanya kitu hata kama siyo shambulizi kamili na inawezekana zaidi itaendelea kushambulia kwa njia ya hali ya juu ya kisaikolojia na mchanganyiko wa tishio la kivita ambapo imekuwa ikitumia dhidi ya Ukraine na Ulaya ikiongeza kasi hiyo kwa muongo uliopita na hata zaidi.

Rais wa Ukraine amekuwa akiomba utulivu kabla ya mkutano wa Jumatano ukiwashirikisha maafisa wa Ukraine, Russia, Ujerumani na Ufaransa – maarufu kama “Normandy format” – kujadili kwa mara nyingine mkoa wa Donbass wa mashariki mwa Ukraine, ambako karibu nusu ya eneo hilo linakaliwa kwa mabavu tangu 2014 na wanajeshi wa Russia na wanajeshi mamluki wa eneo hilo.

Alipoulizwa katika mkutano wa waandishi wa habari wa kigeni Ijumaa juu ya tathmini mbalimbali na uwezekano wa kutoelewana na Biden, Zelenskiy alieleza wasiwasi wake juu ya uchumi wa Ukraine, akisema kuwa kuzungumzia uvamizi usiokuwa na mashaka unaathari sana uchumi. “Kwangu mimi, swali la kuwepo uwezekano wa kusambaa kwa mivutano siyo umuhimu kwa upande wa Marekani na washirika wengine,” alisema.

Lakini alilalamika kuwa vyombo vya habari vilikuwa vinatoa taswira kuwa tuna majeshi mitaani na “hivyo sivyo ilivyo.” Alisema Ukraine “haihitaji taharuki kama hii” kwa sababu inaharibu uchumi. “Tunaweza kupoteza uchumi tulio nao hivi sasa.” Aliongeza.

Kiongozi wa Ukraine alililenga suala hilo wiki iliyopita wakati Marekani, Uingereza, Canada na Australia walipotangaza kuondoa wafanyakazi wake kutoka balozi zao. Zelenskiy na washauri wake walielezea kufadhaishwa na hilo, wakisema kuondolewa kwa baadhi ya wafanyakazi wa balozi kulifanywa kwa haraka.

Afisa mmoja aliiambia VOA kuwa kuondoshwa kwa wafanyakazi kunadumaza juhudi za kutuliza hofu ya wananchi wa kawaida wa Ukraine. Marekani na Uingereza nao pia zimewaambia raia wao kuondoka Ukraine.

XS
SM
MD
LG