Wakati huohuo kumekuwa na mapigano makali ya barabarani katika mitaa kwenye mji muhimu wa Severodonetssk na Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema kwamba sehemu kubwa ya jiji hilo sasa iko mikononi mwa Russia.
Baada ya takriban siku 100 za mapigano vikosi vya Russia sasa vinadhibiti asilimia 20 ya nchi, hiyo ni kulingana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky katika hotuba aliyoitoa kwenye bunge la Luxembourg.
Msemaji wa walinzi wa kitaifa wa Ukraine alisema Kyiv inafanya kila juhudi kuwazuiya maadui, hata kama wapiganaji wake 100 wanauwawa kila siku huko severodonetsky.
Jamhuri ya watu wa Luhansky inayoungwa mkono na Russia inasema kuwa sasa inadhibiti eneo lote la Luhansk isipokuwa miji ya severodonetsk na Lysychansk.