Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 29, 2024 Local time: 07:44

Mwandishi wa ufaransa auwawa kufuatia mashambulizi ya mabomu ya Russia

Mwandish wa habari wa Ufaransa Frederic Leclerc-Imhoff ameuwawa huko Ukraine katika jimbo la Luhansk.(Reuters).
Mwandish wa habari wa Ufaransa Frederic Leclerc-Imhoff ameuwawa huko Ukraine katika jimbo la Luhansk.(Reuters).

Maafisa wa ufaransa na Ukraine wamesema, Mwandishi wa ufaransa ameuwawa jumatatu kufuatia mashambulizi ya mabomu ya Russia yaliyopiga gari lililokuwa linawahamisha raia kutoka mashariki mwa Ukraine. 

Maafisa wa ufaransa na Ukraine wamesema, Mwandishi wa ufaransa ameuwawa jumatatu kufuatia mashambulizi ya mabomu ya Russia yaliyopiga gari lililokuwa linawahamisha raia kutoka mashariki mwa Ukraine.

Frederic Leclerc-Imhoff alikuwa Ukraine kuonyesha jinsi vita vilivyo, aliandika hayo rais wa ufaransa Emmanuel Macron katika mtandao wa twitter.” Leclec –Imhoff alikuwa anafanya kazi katika shirika la habari la televisheni la BFM ambalo limesema alikuwa na umri wa miaka 32 na ilikuwa safari yake ya pili huko Ukraine kwa ajili ya kuripoti tangu vita vilipoanza Februari 24, mwaka huu. Alikuwa karibu na mji wa Severodonetsk mji ulioko mashariki mwa Ukraine ambao umekabiliwa na mashambulizi ya Russia yanayoendelea katika wiki za karibuni, wizara za mambo ya nje za Ukraine na ufaransa zimesema katika taarifa tofauti. Waziri wa mambo ya nje Catherine Colonna aliyeitembelea Kyiv jumatatu alisema katika mtandao wake wa Twitter kwamba Leclerc –Imhoff ameuwawa , na mashambulizi ya mabomu ya Russia katika ujumbe wa kibinadamu wakati akifanya kazi yake ya kutoa taarifa.

XS
SM
MD
LG