Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 27, 2024 Local time: 05:49

Uganda yawaachia huru raia 9 wa Rwanda katika kesi ya ujasusi


Rais Paul Kagame (Kushoto) na Rais Yoweri Museveni
Rais Paul Kagame (Kushoto) na Rais Yoweri Museveni

Uganda imeawaachilia huru wafungwa tisa raia wa Rwanda ambao walikuwa wanazuiliwa nchini humo kwa mashtaka ya kufanya ujasusi kwa niaba ya serikali ya Rwanda na kumiliki silaha kinyume cha sheria.

Serikali ya Uganda inasema hatua hiyo imechukuliwa ili kurejesha uhusiano mwema na Rwanda, huku juhudi za kidiplomasia zikiendelea kati ya nchi hizo mbili jirani.

Katika hafla ya kuwapokea raia hao tisa kwa balozi wa Rwanda nchini Uganda Frank Mugambage, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Sam Kutesa amesema kuachiliwa kwa raia hao tisa, sio kwa sababu hawana makosa na kufutilia mbali madai kwamba walikamatwa kiholela inavyodai serikali ya Rwanda.

Kutesa amesisitiza kwamba raia hao wanaweza kukamatwa tena endapo maafisa wa Uganda watahisi wanastahili kuwajibishwa.

Hatua hii ni ishara ya nia njema ya kutaka uhusiano mwema kati ya nchi hizi mbili. Tuna matumaini kwamba Rwanda itafuata njia hii katika kurejesha uhusiano mwema jinsi ilivyokuwa awali, amesema Kutesa.

Miongoni wa walioachiliwa huru na mahakama ya kijeshi ya Makindye, jijini Kampala, ni pamoja na Sagenti Rene Rutagungira, ambaye amekuwa akitajwa sana katika mgogoro wa Rwanda na Uganda, aliyekamatwa kwa madai ya kumkamata na kumrejesha Rwanda aliyekuwa mmoja wa walinzi wa rais Paul Kagame Lt Joel Mutabazi.

Wengine ni Bahati Mugenga, Emma Rwamuco, Augustine Rutisiri, Etiene Nsanzabahizi, Charles Byaruhanga na Claude Iyakaleme.

Walikuwa wakikabiliwa na mshtaka ya kuifanyia ujasusi Rwanda, kumiliki silaha kinyume cha sheria, na kupanga njama za kuipindua serikali ya rais Yoweri Museveni. Serikali ya Rwanda inasema bado kuna idadi kubwa ya raia wake wanaozuiliwa Uganda.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Kennes Bwire, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG