Hii ni baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi, Kale Kayihura, kupitia Mwanasheria Mkuu, kufungua kesi dhidi ya gazeti la Red Pepper, Mchunguzi, Repoti za Chimp na wahariri binafsi kuhusiana na suala hilo.
Generali Kayihura anawatuhumu washtakiwa hao kwa kuchapisha repoti ya siri inayohusiana na uchunguzi huo na usalama wa Uganda bila ya kupata ruhusa ya polisi.
Amedai kuwa machapisho hayo yamevuruga uchunguzi, usalama wa taifa na kuharibu shughuli za vyombo vya usalama nchini Uganda.
Amri hiyo ya mahakama itatekelezwa kuanzia Agosti 21, 2017 wakati ambazo kesi ya msingi itaposikilizwa mbele ya Jaji Stephen Musota.
Kaweesi, Erau na Wambewo waliuawa Machi 17, 2017 na watu wasiojulikana wakati wakiondoka nyumbani kwa kamanda huyo huko Kulambira