Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 17:51

Timu ya wanasheria wa Trump kupinga amri ya kiwango cha kutoa habari


Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump akikabiliwa na mashtaka kadhaa katika mahakama ya serikali kuu mjini Washington.
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump akikabiliwa na mashtaka kadhaa katika mahakama ya serikali kuu mjini Washington.

Ni ‘uongo’ ndivyo rais wa zamani Donald Trump, anayewania tena uteuzi wa kugombea urais, ameelezea mashtaka ya karibuni wakati alipoongea siku ya Jumamosi mbele ya wafuasi wake huko Columbia, South Carolina.

Wiki iliyopita, alifika mahakamani kwa shutuma za kupanga njama za kubadili matokeo ya uchaguzi wa rais alioshindwa mwaka 2020.

Upande wa mashtaka utakuwa na wakati mgumu kuthibitisha, alidai wakili wa Trump, Joyn Lauro, kwenye kituo cha televisheni cha ABC katika kipindi cha “This Week.” “Iwe alikuwa anafanya ufisadi au la. Iwe alikuwa anatenda kwa dhamiri ya nia ya uhalifu au la. Hawataweza kuthibitisha.”

FILE PHOTO: Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump akiwa mahakamani mjini Washington.
FILE PHOTO: Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump akiwa mahakamani mjini Washington.

Baada ya Trump kuposti kwenye mtandao kile kilichoonekana kuwa ni ahadi ya kulipiza kisasi kwa yeyote ambaye anamfuatilia, waendesha mashtaka walimuuliza jaji wa serikali kuu kuweka kizuizi kwa Trump na timu yake kutoa habari kwa umma kuhusu kesi yake. Timu ya kisheria ina mpaka Jumatatu kujibu. Lauro alisema hayo kwenye kituo cha televisheni cha CNN.

Lauro anaongezea, “vyombo vya habari na watu wa Marekani katika msimu wa kampeni wana haki ya kufahamu kuna ushahidi gani katika kesi hii, ilimradi ushahidi huo hauna kizuizi, kwahiyo tutapinga hilo.”

Makamu Rais wa zamani Mike Pence, ambaye pia ni mgombea urais mtarajiwa na huenda akaitwa kutoa ushahidi katika kesi, alielezea kwenye CNN kwanini alipinga maombi ya mawakili wa Trump kubadili matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020. “Hakuna makamu rais au mtu yeyote anatakiwa kuwa na haki ya kuchagua rais wa Marekani. Urais ni wa watu wa Marekani pekee.”

Makamu wa Rais wa zamani Mike Pence
Makamu wa Rais wa zamani Mike Pence

Majibu ya ulimwengu kwa changamoto za kisheria za Trump yameonyesha kuwa ya kasi ya pole pole. James Long, profesa wa sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Washington, hashangazwi na hilo.

“Baadhi ya viongozi katika nchi maalum, wamekuwa wakiangalia ujumbe usio sahihi kutokana na tabia ya Trump hadi sasa. Lakini nadhani hivi sasa, kwa kweli wenye busara wamekaa kimya na kuachia mchakato uendelee na kujaribu kuwa na uhusiano mzuri wa kidiplomasia na Marekani,” anasema Long.

Ingawaje watu huko nje huenda wakawa wamechoka kusikia kuhusu hilo au wanafikiri huenda lina matokeo yake, mashtaka ya karibuni ya Trump ni lazima yachukuliwe kwa dhati, kwa mujibu wa Kathryn Sikkink, mtalaamu wa uhusiano wa kimataifa katika Shule ya Havard Kennedy.

“Kama huna demokrasia au demokrasia ni dhaifu, haki za binadamu ziko hatarini. Kwahiyo naamini kwamba katika muda mrefu ujao, kama hili litashughulikiwa vyema nchini Marekani, nchi nyingine nazo zitalipa uzito.”

Katika maoni yake, suala hilo limekuwa ni mfano wa jinsi Marekani ina uwezo wa kukabiliana na matatizo yake, kwa kutumia sheria.

Forum

XS
SM
MD
LG