Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:09

Trump akabiliwa na mashtaka mengine ya uhalifu yanayohusiana na uchaguzi wa 2020


Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump akizungumza wakati wa kampeni ya uchaguzi wa 2024 katika mji wa Erie, jimbo la Pennsylvania, Julai 29, 2023.
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump akizungumza wakati wa kampeni ya uchaguzi wa 2024 katika mji wa Erie, jimbo la Pennsylvania, Julai 29, 2023.

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump Jumanne amekabiliwa na mashtaka mengine ya uhalifu kwa mara ya tatu katika kipindi cha miezi minne, mashtaka ya hivi sasa yanahusiana na juhudi zake za kutaka kubatilisha uchaguzi wa 2020 ambao alishindwa.

Mashtaka hayo manne yanadai kuwa Trump alipanga njama ya kuilaghai Marekani kwa kulizuia Bunge kurasmisha ushindi wa Rais Joe Biden na kuwanyima wapiga kura haki yao ya uchaguzi wa haki.

Trump ameamriwa kufika katika mahakama ya serikali kuu Alhamisi.

Mashtaka hayo yanadai kwamba Trump alikula njama na watu wengine sita ambao majina yao hayakutajwa kwa kutaka kubadili matokeo ya uchaguzi.

Waendesha mashtaka waliandika kwamba Trump alijua madai yake kwamba uchaguzi ulikuwa na wizi yalikuwa ya uongo, lakini aliyarudia hata hivyo ili “kuleta hali ya kutoaminiana na hasira ndani ya taifa na kuondoa imani ya umma katika usimamizi wa uchaguzi.

Katika taarifa, timu ya kampeni ya Trump imesema Trump amekuwa akifuata sheria kila mara na kuyataja mashtaka hayo kama “unyanyasaji” wa kisiasa kama ule wa enzi ya Unazi wa Ujerumani.

Forum

XS
SM
MD
LG