Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 23:12

Waendesha mashitaka wa Marekani waongeza wigo wa kesi yao ya jinai dhidi ya Donald Trump

Rais wa zamani Donald Trump akipunga mkono kabla ya kupanda ndege yake ya kibinafsi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Miami, Jumanne, Juni 13, 2023, huko Miami.
Rais wa zamani Donald Trump akipunga mkono kabla ya kupanda ndege yake ya kibinafsi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Miami, Jumanne, Juni 13, 2023, huko Miami.

Waendesha mashitaka wa Marekani waliongeza wigo wa kesi yao ya jinai dhidi ya Donald Trump siku ya Alhamisi huku wakimshtaki mfanyakazi wake wa pili kwa kumsaidia rais huyo wa zamani kuwakwepa maafisa waliokuwa wakijaribu kupata  nyaraka  nyeti za usalama wa taifa alizochukua kutoka Ikulu.

Mwendesha mashitaka maalum Jack Smith alimshtaki Carlos De Oliveira, mfanyakazi ambaye ni fundi katika nyumba ya Trump ya Mar-a-Lago huko Florida kwa njama ya kuingilia kati sheria, kutoa taarifa za uongo na kuharibu nyaraka.

Wakili wake hakujibu mara moja ombi la kutoa maoni yake.

Vyombo vya habari vimesema kuwa De Oliveira alisaidia kuficha nyaraka hizo kutoka kwa maafisa waliokuwa wakijaribu kuzichukua.

Forum

XS
SM
MD
LG