Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 16:55

Tanzania: Polisi wamwachia huru Dr Wilbroad Slaa na watu wengine wawili


DR Wilbroad Slaa (Kwa hisani ya Akaunti ya Dr Slaa ya Facebook)
DR Wilbroad Slaa (Kwa hisani ya Akaunti ya Dr Slaa ya Facebook)

Jeshi la Polisi nchini Tanzania Ijumaa limemuachia huru mwanadiplomasia mstaafu Wilbroad Slaa baada ya kushikiliwa kwa siku kadhaa.

Mwanadiplomasia huyo na watu wengine wawili walikamata kwa madai ya uchochezi.

Bado haiko bayana misingi gani ilipelekelea kuachiliwa kwake; juhudi za kumfikia wakili wake, Dickson Matata hazikuzaa matunda kwani simu yake ilikuwa haijibiwi.

Lakini vyanzo kadhaa ndani ya jeshi la polisi katika kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es salaam vilithibitisha kuwa mwanadiplomasia huyo machachari alikuwa ameachiwa.

Wakati huo huo Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Tanzania Ijumaa limetoa tamko kuitaka serikali isikilize kilio cha wananchi kuhusu kero kwa mkataba uliosainiwa kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na “Emirates of Dubai” juu ya ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa maendeleo na uboreshaji wa bandari za Bahari na za Maziwa Tanzania.

Katika wakaraka huo ambao umesainiwa na Maaskofu 37 unaeleza: “Sisi Maaskofu Katoliki Tanzania wenye jukumu la kusimamia ustawi wa kila mwanadamu tunamuomba Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania, kwa mamlaka aliyo nayo asitishe wasilisho la ridhio hili kwa upande wa pili, na vile vile Bunge nalo lifute ridhio la Mkataba huu unaolalamikiwa,” umeeleza waraka huo.

“Tukisukumwa na dhamiri iliyo na lengo la kulinda rasilimali, mshikamano, amani, uhuru, na umoja wa kitaifa; tunathubutu kusema kuwa baada ya miaka 63 ya uhuru wa nchi hii, wananchi hawajapenda kuiachia bandari ya Dar es Salaam apewe mwekezaji mmoja aiendeshe, kwa vile Watanzania wenyewe wana uzoefu wa kuiendesha,” waraka huo umeeleza.

Waraka huo unaeleza pia: “Tumefuatilia kwa umakini mijadala, maoni, mapendekezo na vilio vya wananchi walio wengi, ambao ni wamiliki wa bandari na rasilimali zote, na tumetambua kuwa wananchi walio wengi hawautaki Mkataba huu ambao unampa mwekezaji wa nje mamlaka na haki ya kumiliki njia kuu za uchumi kama zilivyobainishwa kwenye mkataba huu.”

Habari hii inatokana na gazeti la The Citizen na vyanzo vingine vya habari Tanzania.

Forum

XS
SM
MD
LG