Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 14:51

Polisi nchini Tanzania wawakamata wakili na mwanasiasa wa upinzani kwa kuandaa maandamano


Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa Bujumbura, tarehe 4, Februari 2023.Picha na Tchandrou Nitanga / AFP.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa Bujumbura, tarehe 4, Februari 2023.Picha na Tchandrou Nitanga / AFP.

Polisi nchini Tanzania wamewakamata wakili na mwanasiasa wa upinzani wakiwashtumu kwa uchochezi na kupanga kuandaa maandamano ya nchi nzima yenye lengo la kuiangusha serikali.

Polisi walimkamata wakili Boniface Anyasile Mwabukusi na Mpaluka Nyagali siku ya Jumamosi, msemaji wa polisi David Misime alisema katika taarifa.

Philip Mwakilima, wakili anayewawakilisha wawili hao waliokamatwa, ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba alikuwa akifanya juhudi kupata fursa ya kuwaona wakiwa chini ya ulinzi na kwamba tuhuma dhidi yao ni “uongo, uzushi.”

Mkuu wa polisi wa Tanzania Camillus Wambura alisema katika taarifa siku ya Ijumaa kwamba anachukua hatua dhidi ya kundi linalopanga kufanya maandamano nchini kote ili kuiangusha serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kabla ya mwaka 2025.

Alisema kuna ujumbe uliochapishwa kwenye mitandao ya kijamii tangu Agosti 10 ili “kuwashawishi na kuwachochea” Watanzania kufanya maandamano ya nchi nzima.

Mmoja wa ujumbe huo ulisema wataipindua serikali ya rais kabla ya mwaka 2025. Huu ni uhaini, alisema mkuu wa polisi Camillus Wambura.

Forum

XS
SM
MD
LG