Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 06:49

Kamata kamata Tanzania kwa wanaopinga mkataba wa bandari


Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa Bujumbura, tarehe 4, Februari 2023.Picha na Tchandrou Nitanga / AFP.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa Bujumbura, tarehe 4, Februari 2023.Picha na Tchandrou Nitanga / AFP.

Polisi nchini Tanzania wamewakamata wakili mmoja na mwanasiasa wa upinzani, wakiwahutumu kwa kuchochea na kupanga maandamano kote nchini humo kwa lengo la kuiangusha serikali.

Wakili Boniface Anyasile Mwabukusi na Mpaluka Nyagali walikamatwa jumamosi.

Wakili Mwabukusi, alikuwa miongoni mwa mawakili waliowasilisha kesi mahakamani kupinga mkataba huo, na kesi ilitupiliwa mbali alhamisi wiki iliyopita. Amesema atakata rufaa.

Wakili wa wawili hao, Philip Mwakilima, ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba alikuwa anafanya kila juhudi kuzungumza na wateja wake wanaozuliwa na polisi, na kwamba madai dhidi yao ni ya uongo.

Mkuu wa polisi wa Tanzania Camillus Wambura amesema katika taarifa kwamba anachukua hatua dhidi ya kundi lililokuwa linapanga kuandaa maandamano kote nchini humo, kwa lengo la kuuangusha utawala wa rais Samia Suluhu Hassan kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Amesema kwamba wawili hao wamekuwa wakiandika ujumbe kwenye mitandao ya kijamii tangu tarehe 10 mwezi Agosti, wakiwa na lengo la kuchochea na kuwashawishi raia wa Tanzania kufanya maandamano kote nchini, na kwamba mmoja wao alisema kwamba wataipindua serikali ya rais kabla ya uchaguzi mkuu, jambo ambalo ni uhaini.

Wambura amesema kwamba wanaoitisha maandamano wanapinga maamuzi ya mahakama kutupilia mbali kesi inayopinga mkataba kati ya serikali na kampuni ya Dubai ya DP World kuhusiana na usimamizi wa bandari ya Dar-es-salaam. Bunge la Tanzania liliidhinisha mkataba huo mnamo mwezi June.

Watetezi wa haki za binadamu wamesema kwamba watu 22 wanazuiliwa na polisi au kutishiwa tangu mwezi June kwa kulikosoa bunge baada ya kuidhinisha mkataba kati ya serikali na DP World.

Msemaji wa serikali Gerson msigwa amepuuza madai kwamba serikali inawanyamazisha wanasiasa wa upinzani kwa nguvu.

Forum

XS
SM
MD
LG