Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 07:45

Tanzania na Oman zakubaliana kushirikiana katika uwekezaji


Rais Samia suluhu Hassan
Rais Samia suluhu Hassan

Oman na Tanzania zimekubaliana kuwekeza pamoja kwa ajili ya kusaidia sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, uvuvi na madini.

Shirika la habari la serikali ya Oman limemnukuu Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Badr al- Busaidi akisema hayo leo.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan yuko katika ziara ya kikazi nchini Oman.

Mapema jumatatu asubuhi, Sultani Haitham Bin Tarik alifanya mazungumzo ramsi na Rais Samia.

Mazungumzo hayo yalizingatia ushirikiano wenye nguvu baina ya nchi hizo mbili na jinsi ya kuinua mahusiano hayo kwa ajili ya manufaa ya watu wa Tanzania na Oman.

XS
SM
MD
LG