Marufuku hiyo iliwekwa mwaka 2016, ili kulinda wanyama na ndege wanaolindwa nchini humo ambao walikuwa wakisafirishwa nje ya nchi kinyume cha sheria.
Hata hivyo Jumamosi, mamlaka ya wanyamapori ilitangaza kuwa ingeondoa marufuku hiyo kwa muda wa miezi sita kuanzia tarehe 6 Juni hadi tarehe 5 Disemba kwa wafanyabiashara kuondoa “akiba ya wanyama” ambao hawakuweza kuwauza kwa sababu ya marufuku hiyo.
Lakini katika kubadili msimamo kwa haraka, waziri wa utalii Pindi Chana aliirejesha marufuku hiyo ili kuruhusu mashauriano zaidi.
“Kulikuwa tangazo ambalo linaruhusu usafirishaji wa wanyamapori nje ya nchi lakini kama waziri muhusika, nimesimamisha hatua hiyo mara moja,” amesema.
Uamuzi wa kuondoa marufuku hiyo ulizua ukosoaji mkubwa kwenye mitandao, huku Watanzania wengi wakitaka upitiwe upya.