Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 01:23

Tanzania: Mkuu wa Mkoa aunda kamati kuchunguza tukio la moto Soko la Karume


Soko la Kariakoo : Moto wateketeza Soko la Karume, Dar es Salaam (Kwa Hisani ya Michuzi TV)
Soko la Kariakoo : Moto wateketeza Soko la Karume, Dar es Salaam (Kwa Hisani ya Michuzi TV)

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), Amos Makalla amewataka wafanyabiashara wa soko la Karume lililoungua kuwa watulivu alipotembelea eneo la tukio kukagua athari za moto Jumapili na kuahidi kuunda kamati itakayochunguza chanzo cha moto huo.

Soko la Karume liliteketea usiku wa kuamkia Jumapili huku chanzo cha moto huo kikiwa hakijulikani.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari soko hilo lenye wafanyabiashara zaidi ya 3,500 moto ulianza usiku wa kuamkia Jumapili huku kikosi cha zimamoto kikikabiliana kuuzima lakini uliteketeza sehemu kubwa ya soko hilo.

Makalla aliwafariji wote walioathiriwa na moto huo akisema: "Nawapa pole wafanyabiashara wote kwa ajali ya moto hatujajua chanzo kwa kuwa yanaelezwa mengi, wengine wanasema umesababishwa na watu wanaopika maharage usiku ili ikifika asubuhi yameiva. Nawaomba kuweni watulivu katika kipindi hiki ambacho tunaunda kamati itakayochunguza kujua chanzo.”

“Tutaunda kamati itakayoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala kuchunguza kwa siku 14 kisha tutapokea majibu na kujua cha kufanya na wakati wote wa uchunguzi hakuna mfanyabiashara atakayeruhusiwa kuendelea na biashara katika eneo hili tutaangalia utaratibu mwingine,"amesema.

Chanzo cha habari hii ni gazeti la mwananchi na vyanzo vingine, Tanzania.

XS
SM
MD
LG