Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 20, 2024 Local time: 00:46

Talibani yapiga marufuku sauti na sura za wanawake kuonekana hadharani


Wanawake wa Afghanistan wakitembea sokoni huko Kandahar Agosti 24, 2024. Picha na Wakil KOHSAR / AFP.
Wanawake wa Afghanistan wakitembea sokoni huko Kandahar Agosti 24, 2024. Picha na Wakil KOHSAR / AFP.

Watawala wa Talibani wamepiga marufuku sauti na sura za wanawake kuonekana hadharani kwa mujibu wa sheria mpya iliyoidhinishwa na kiongozi mkuu katika juhudi za kupambana na uovu na kukuza tabia njema.

Sheria hiyo iliyopitishwa siku ya Jumatano, baada ya kuidhinishwa na kiongozi mkuu Hibatullah Akhundzada, msemaji wa serikali imesema. Talibani imeunda wizara kwa ajili ya uenezi wa tabia njema na kuzuia maovu” baada ya kuchukua madaraka mwaka 2021.

Wizara hiyo imechapisha sheria zake za mema na maovu siku ya Jumatano ambazo zinashughulikia nyanja za maisha ya kila siku kama vile usafiri wa umma, muziki, kunyoa na hafla.

Wameainisha katika waraka wa kurasa 114, wa vifungu 35 ulioonekana na shirika la habari la Associated Press na tangazo la kwanza rasmi la sheria za mema na maovu nchini Afghanistani tangu iingie madarakani.

Sheria hiyo inaipa wizara mamlaka ya kuwa mstari wa mbele katika kudhibiti mienendo binafsi , kutoa adhabu kama vile onyo au kukamatwa ikiwa watekelezaji wakidai Waafghanistan wamekiuka sheria.

Kifungu cha 13 kinachohusiana na wanawake, kinasema ni lazima wanawake kujifunika mwili wakati wote wakiwa hadharani na kufunika uso ni muhimu kuepuka majaribu na kuwajaribu wengine. Nguo zisiwe nyepesi, zinazobana au fupi.

Kifungu cha 17 kinapiga marufuku picha za viumbe hai, na kutishia hali ya vyombo vya habari vya Afghanistan ambavyo tayari ni tete.

Kufungu cha 19 kinapiga marufuku kucheza muziki, usafiri wa umma wa wanawake kusafiri peke yao, na kuchanganyika na wanaume na wanawake ambao hawana undugu.

Forum

XS
SM
MD
LG