Waziri wa Mambo ya Nje wa Taliban, Amir Khan Muttaqi, aliuambia mkutano wa kitaifa wa wafanyikazi mjini Kabul kwamba nchi yake ilikuwa mzalishaji na msambazaji mkubwa zaidi duniani.
Amesema ilikuwa ni jambo la hatari kwa kuwa dawa za kulevya zilisafirishwa duniani kote na kusababisha zaidi ya Waafghanistan milioni 4 kuishi na uraibu kwa miongo miwili iliyopita.
Kwa kuwa uzalishaji huo umekwisha, Waraibu hao sasa wanahitaji matibabu huku wakulima wakihitaji riziki nyingine na ajira, amesema Muttaqi, katika hotuba yake kwa njia ya televisheni.
Kampeni yao amedai, imesababisha shinikizo kubwa la kiuchumi.
Forum