Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 00:34

Taifa la Palestina huenda likaondolewa nguvu za kijeshi


Muandamanaji wa Palestina akikimbia wakati wa makabiliano na wanajeshi wa Israel katika mji Al-Bireh Oktoba 27, 2023. Picha na Aris MESSINIS / AFP
Muandamanaji wa Palestina akikimbia wakati wa makabiliano na wanajeshi wa Israel katika mji Al-Bireh Oktoba 27, 2023. Picha na Aris MESSINIS / AFP

Hatma ya Palestina inaweza kuondolewa nguvu za kijeshi na kuwepo kwa vikosi vya kimataifa kwa usalama kwa muda ili kutoa dhamana kwa Palestina na Israel, Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi alisema Ijumaa.

"Tulisema tuko tayari kwa hali hii ya kutokuwa na nguvu za kijeshi, na kunaweza pia kuwa na dhamana ya vikosi, iwe vya NATO, vya Umoja wa Mataifa, au Kiarabu au vya Marekani , hadi usalama upatikane kwa pande zote mbili, kwa mataifa mapya ya Palestina na Israeli," Sisi alisema wakati wa mkutano wa pamoja mjini Cairo akiwa na Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez pamoja na Waziri Mkuu wa Ubelgiji Alexander De Croo mbele ya waandishi.

Azimio la kisiasa ambalo linataka taifa la Palestina liwepo kulingana na mipaka ya Juni 4, 1967, na Jerusalemu Mashariki kama yake mji mkuu wake, umebakia kuwa nje ya maafikiano, aliongeza Sisi.

Mataifa ya Kiarabu yamekataa mapendekezo kwamba jeshi la Kiarabu kutoa usalama huko Ukanda wa Gaza, baada ya kusitishwa operesheni ya sasa ya kijeshi ya Israel dhidi ya kundi wanamgambo wa Palasetina Hamas. Israel imekuwa ikiidhibiti Gaza tangu 2007.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan Ayman Safadi aliwaambia waandishi wa habari mjini London wiki hii kwamba mataifa ya Kiarabu yasingetaka kuingia Ukanda wa Gaza ambao unaweza kugeuzwa kuwa "nyika" ya mashambuzi ya jeshi la Israel.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG