Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 00:37

Sitisho la mapigano Gaza: Hali ya utulivu yaripotiwa katika mpaka wa Lebanon



Moto na moshi katika eneo la Khiam kusini mwa Lebanon Novemba 23, 2023. Picha na HASSAN FNEICH / AFP.
Moto na moshi katika eneo la Khiam kusini mwa Lebanon Novemba 23, 2023. Picha na HASSAN FNEICH / AFP.

Hali ya utulivu ilirejea katika mpaka wa kusini mwa Lebanon siku ya Ijumaa wakati sitisho la mapigano la muda likiana kutekelezwa katika vita kati ya Israel na Hamas huko Gaza, kulingana na vyombo vya habari vya serikali ya Lebanon na jeshi la Israel.

Tangu vita vya Gaza vilipozuka tarehe 7 Oktoba, mpaka wa kusini mwa Lebanon na Israel umeshuhudia kurushiana risasi, hususani kati ya jeshi la Israel na kundi la Hezbollah la Lebanon, pamoja na makundi ya wapiganaji wa Palestina.

Hezbollah bado haijasema kama itazingatia misingi ya makubaliano hayo ambayo yalisimamiwa na Qatar kwa msaada kutoka Misri na Marekani.

"Utulivu huo ambao hauna uhakika, ulitawala kwenye mpaka wa kusini, na usitishaji wa amani wa kibinadamu huko Gaza ulianza kutekelezwa saa moja asubuhi " Shirika rasmi la Habari la Lebanon liliripoti.

Saa sita baada ya sitisho hilo huko Gaza kuanza kutekelezwa, msemaji wa jeshi la Israel alilithibitishia kwa shirika la habari la AFP kwamba hadi sasa hakuna matukio yoyote yaliyofuata au ufyatuaji risasi katika mpaka wa Lebanon.

Mwandishi wa habari wa AFP katika eneo la mpaka la Marjayoun alisema milio ya kurushiana risasi ilisikika dakika 10 kabla ya sitisho hilo, kabla ya milio hiyo ya bunduki kunyamaza.

Siku ya Ijumaa, kundi lenye nguvu la Kishia linaloungwa mkono na Iran lilidai kuhusika na mashambulizi 22 kwenye maeneo ya Israel kutoka kusini mwa Lebanon, ambapo lilipoteza wapiganaji wake saba mchana huo.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG