Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:28

Spika awataka mawaziri kujibu tuhuma za upinzani mitandaoni


Bunge la Tanzania
Bunge la Tanzania

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, amewataka mawaziri kuwafuata wabunge wa upinzani huko kwenye mitandao ya kijamii na kuwajibu.

Gazeti la Mtanzania limeripoti kuwa amesema imekuwa ni kawaida kwa wabunge wa upinzani kuchokoza Serikali kwa kuuliza maswali bungeni, na wanapotoka nje hurusha video zao mitandaoni.

Akizungumza bungeni wiki hii, Ndugai alisema. “Mtaona kuna katabia kana muda sasa ka watu wanachokoza, wanaisema serikali weee, inapofika muda Serikali kujibu wao ‘wanachimba’, wanatoka humu ndani.

“Wanapotoka humu ndani kuna watu wao tayari wanachukua clip (video) tayari wanarusha kwenye Youtube, Youtube inapoangaliwa nchi nzima, dunia nzima wanaona mawazo yale, utamzuiaje Mtanzania yeyote kuwaamini wale kwamba walichosema ndicho chenyewe?

“Lakini na ninyi upande wa Serikali hakuna clip utakayo iona sijui ya AG (Mwanasheria Mkuu wa Serikali) au Profesa Kabudi (Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi) akielezea hayo mambo, hakuna kwa hiyo sasa twendeni kisasa, wanavyoenda wao twendeni hivyo hivyo tuwakute huko huko, eeh na wanafanikiwa sana kuidanganya jamii,” alisema Spika Ndugai.

Katika hatua nyingine, amelifananisha Bunge lake na utawala wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete baada ya wabunge wa Chadema, Halima Mdee na Cecil Mwambe kudai mhimili huo unaingiliwa na Serikali.

Ndugai alisema hata awamu ya Kikwete wabunge hao walikuwa wanaiponda hivyo hata mabunge yajayo watafika mahali na kusema bora lilivyo Bunge la sasa.

XS
SM
MD
LG